SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAZINDUA MAUZO YA NYUMBA ZAKE ZA VICTORIA PLACE, DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifanya mahojiano na Ephraim Kibonde wa Kipindi cha Maisha ni Nyumba cha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Michael Chilongani wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwafafanulia jambo wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwafafanulia jambo wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Abdulkarim Shah akibadilishana mawazo na wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Sophia Mwema wa Shirika la Nyumba la Taifa akibadilishana mawazo na mmojawapo wa wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu akijadiliana jambo na mwenzake kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Gibson Mwaigomole wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwafafanulia jambo wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
David Shambwe, Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara, David Shambwe akishuhudia namna shughuli hiyo inavyoendelea. Picha zaidi za tukio hili tutawaletea.
.......................................................................................................................
TAARIFA YA UUZWAJI WA NYUMBA ZA VICTORIA PLACE, DAR ES SALAAM
Kwa mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo (Ijumaa, 6, Machi, 2015) limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Victoria, jijini Dar es Salaam. Mradi unatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya Sh 11 bilioni mpaka utakapomalizika.
Mradi huu upo Victoria Kijitonyama, takribani kilomita 7 kutoka Jijini Kati, una nyumba 127 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo pacha ya ghorofa 13. Mradi huu uko sehemu yenye huduma zote muhimu za kijamii jijini Dar es Salaam zikiwamo za kiafya, shule, maduka, na masoko. Mbali na huduma katika ujirani, mradi wenyewe utakuwa na maeneo ya biashara katika ghorofa ya chini (ground floor) na ghorofa ya kwanza, ambapo tunatarajia kuwepo na huduma nyingine za kijamii kama vile “Supermarkets”, Migahawa n.k
Kadhalika, Mradi huu unatarajiwa kuboresha maisha ya wanunuzi wa nyumba hizi kwani umejikamilisha kwa huduma za wakazi,kwa kuwa na maeneo mawili ya , mazoezi (gym), mabwawa ya kuogelea mawili (swimming pools) na eneo la watoto kuchezea.Zaidi ni kwamba, nyumba zipo ndani ya uzio kwa ajili ya usalama watumiaji na kuna maegesho ya magari ya kutosha.
Mradi una nyumba 127 tu zinazouzwa, zenye ukubwa tofauti, idadi ya vyumba tofauti na bei tofauti. Nyumba hizi zina vyumba kuanzia viwili hadi vinne, na bei zake zinaanzia Tshs165,150,000/= hadi 306,445,000/= kabla ya kodi ya Ongezeko la thamani(VAT). Ukubwa wa nyumba unaanzia mita za mraba 90 hadi 167. Mbali na vyumba vya kulala, kila nyumba ina jiko kubwa la kisasa, choo cha pamoja na eneo la kufulia na kuanikia nguo.
Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalum la kukusanyia taka, sehemu iliyotengwa maalum kwaajili ya kufanyia mazoezi, bwawa la kuogelea na eneo kubwa la ziada la maegesho ya magari.
Nyumba hizi ni Bora na za Kisasa. Tunawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wote walio nchini na walio nje ya nchi, wafanye mawasiliano na makao makuu ya shirika, ofisi zetu za mikoa, au kupitia barua pepe na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU