Ofisa
mwakilishi wa Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Profesa Tolly Mbwette akizungumza
katika hafla maalumu ya uzinduzi wa awamu ya nne ya programu hiyo jana
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa programu hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha
mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar
es Salaam akifundisha kwa washiriki.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiteta
jambo na mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika.
Baadhi
ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha
mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar
es Salaam.

Meza kuu katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai.
Baadhi
ya maofisa toka meza kuu wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa
programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai.
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Taasisi
ya Elimu Tanzania (TIE) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania (OUT) wamewezesha kozi kwa baadhi ya nchi za Afrika yenye lengo
la kuboresha mitaala ya elimu.
Akizungumza kwa niaba ya Naibu
Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela katika hafla ya uzinduzi wa
programu hiyo ya uboreshaji mitaala, aliipongeza UNESCO pamoja na
taasisi zingine zilizounganisha nguvu kuhakikisha kozi hiyo ya
uboreshaji mitaala inafanyika.
Alisema njia pekee ya kuendelea
kuboresha elimu yetu ni kutumia wataalamu wa elimu hasa wanaohitimu
katika kozi maalumu za ubunifu na uandaaji mitaala kuiboresha mitaala
hiyo kwa kuzingatia mahitaji halisi taifa moja hadi lingine.
Alisema awamu ya nne ya mafunzo
hayo ya uboreshaji mitaala ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam
na kujumuisha wanafunzi 100 kutoka nchi 23 ambazo ni pamoja na Uganda,
Kenya, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Zambia, Swaziland, Niger, Senegal,
Cameroon, Burkina Faso, Togo, Chad, Ivory Coast, Nigeria, Hong Kong,
Liberia, Sudan Kusini, Sierra Leone, Benin na wenyeji Tanzania.
Aidha Kilango katika hotuba yake
ameiomba UNESCO pamoja na mashirika wafadhili wa programu hiyo kuangalia
uwezekano wa kuipanua zaidi na kuboresha programu hiyo ili kuwa na
manufaa zaidi jambo ambalo alisema Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano
wowote kufaniisha jambo hilo.
Hata hivyo aliwataka wahitimu wa
mafunzo hayo kutumia nafasi walioipata ipasavyo pamoja na kuifanyia kazi
kitaaluma mara baada ya mafunzo hayo. Alisema elimu ya utaalamu wa
mitaala ni muhimu kwa taifa lolote hivyo kutumia utaalamu walioupata
kuzishauri mamlaka kuboresha elimu kulingana na maitaji.
UNESCO katika hafla hiyo
iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi.
Zulmira Rodrigues ambaye aliwataka wanafunzi watakao pata mafunzo hayo
kutumia elimu ya utaalamu ipasavyo ili kuboresha elimu.
Comments