viongozi wa Siasa hamasisheni wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha katika daftari la Kudumu la wapiga kura-tume ua uchaguzi

       

indexNa Lorietha Laurence-Maelezo
……………………………………………….
Tume ya taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa viongozi wa Siasa kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha katika daftari la Kudumu la wapiga kura na hivyo kupata fursa ya kushiriki katika zoezi la kupiga kura ya maoni Aprili 30 mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam katika taarifa iliyotolewa na Tume hiyo baada ya baadhi ya vyombo vya habari kutoa taarifa za upotoshaji kuhusu mabadiliko ya tarehe ya kupiga kura ya maoni katiba inayopendekezwa.
“kumekuwepo na Taarifa zisizo rasmi zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vikimnukuu Mwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubavu kuwa kuna mabadiliko ya tarehe ya kupiga kura ya maoni wakati taarifa hizo si za kweli na hakuna mabadiliko yeyote kwani tarehe ni ile iliyotangazwa awali ambayo ni tarehe 30 Aprili 2015 ” alisema Kaimu Mkurugenzi wa Tume ni Kailima Ramadhani Kombwey.
Aidha aliongeza kuwa kwa sasa Tume imeweka kipaumbele katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwenye Daftari la kudumu la Wapiga kura kwa kuhakikisha kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 ambaye kwa mujibu wa sheria anaruhusiwa kupiga kura awe amejiandikisha .
“tunawaomba watanzania wenye sifa za kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga Kura wajitokeze na kuweza kujiandikisha na hivyo kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo”alisema Kombwey.
Mkurungezi Kailima alibainisha kuwa endapo zoezi la uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakuwa halijakamilika ifikapo tarehe 30 Aprili 2015 Tume itatoa taarifa rasmi ikiwa ni pamoja na kueleza muelekeo wa zoezi hilo.
Tume imewahakikishia wananchi kuwa hakuna mtu yeyote atakayeachwa kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura endapo atajitokeza kwenye kituo cha kujiandikisha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*