WAMASAI NGORONGORO WALIA MBELE YA KINANA BAADA YA WAZIRI MKUU PINDA KUWAPA AHADI HEWA YA CHAKULA NA WAZIRI MKUU PINDA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia Jamii ya Kimasai katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nainokanoka wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Komredi Kinana ambaye katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, pamoja na mambo mengine alisikiliza pia kero za wananchi hao wanaoishi na Hifadhi ya Ngorongoro ikiwemo ya kutotimiziwa ahadi ya kupatiwa  kila kaya magunia 10 kwa mwaka iliyotolewa na Serikali kupitia kwa WaziriMkuu, Mizengo Pinda.

Pinda inadaiwa aliitoa ahadi hiyo, baada ya Jamii hiyo ya kimasai kupigwa marufuku na Serikali kulima zao lolote  katika maeneo yao wanayoishi ili wasiharibu mazingira ya Hifadhi ya Wanyama ya Ngorongoro.

Kinana ameahidi kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa kukutana mapema iwezekanavyo na Waziri Mkuu Pinda, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na uongozi wa hifadhi hiyo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nainokanoka wilayani Ngorongoro
 Komredi Kinana akigawa mbuzi bure kwa wajane kila kaya mbuzi 15 zilizotolewa na Baraza la Wafugaji Ngorongoro kwa kushirikiana na Hifadhi ya Ngorongoro ili kuwapunguzia watu hao umasikini.



 Mmoja wa akina mama wajane akiswaga mbuzi baada ya kukabidhiwa.
 Komredi Kinana akizungumza na jamii ya kimasai katika Kijiji cha Arashi waliouzuia msafara wake kumueleza kero mbalimbali zinazowakabili ambapo walilalamikiwa ufinyu wa ardhi, kutokuwepo maji katika eneo hilo walilohamishiwa kinguvu baada ya Serikali kuwhamisha eneo lao la awali ililokuwa na mito ili kupisha upanuzi wa Hifadhi ya wanayama. Pia la kuzuka kwa njaa katika eneo hilo linalosababisha pia mifugo yao kufa.
 Komredi Kinana akikaribishwa na Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bruno Kawasange alipowasili Makao Makuu ya Hifadhi hiyo kuzungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji wa Ngorongoro na Mamlaka hiyo.
 Kikundi cha ngoma za asili za Jamii ya Kimasai wakitumbuiza wakati msafara wa Kinana ulipowasili katika Mamlaka  hiyo.


 Komredi Kinana akiangalia ngoma hiyo.

Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro
 Hii ndo Ngorongoro Crater ambapo wanayma wa aina mbalimbali na binadamu wanaishi pamoja
 Komredi Kinana (wa pili kushoto) akishiriki pamoja na viongozi kupaka rangi nyumba ya mganga katika Kijiji cha Bulati wilayani Ngorongoro
 Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro akizungumza  na wananchi katika Kijiji cha Bulati
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda akijitambulisha kwa wananchi katika Kijiji cha Bulati
 Mmiliki wa Blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda akiwa na wamasai katika Kijiji cha Bulati. Mwaikenda ni miongoni mwa wanahabari walio kwenye msafara wa Kinana
 Komredi Kinana na Nape wakiondoka katika Kijiji cha Bulati
 Komredi Kinana akiimbiwa wimbo na akina mama wa kimasai
 Wamasai wakitumbuiza wakati wa mkutano huo
 Kijana mwenye jamii ya kimasai akiwa katika vazi la utamaduni

 Wananchi wakimsikiliza Komredi Kinana akatika Mkutano uliofanyika katika Kata ya Nainokanoka
 Mtoto mwenye jamii ya kimasai mwenye ulemavu wa ngozi, Shungu Sendela anayesoma katika darasa la sita katika Shule ya Msingi ya Nainokanoka wilayani Ngorongoro akiwa miongoni mwa Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kata ya Nainokanoka.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU