ZIARA YA KOMREDI KINANA WILAYA YA BAHI,DODOMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mfereji wa kutandaza mabomba katika mradi wa maji katika Kijiji cha Nguji, Kata ya  Mundemu, wilayani Bahi, wakati wa ziara ya siku tisa mkoani Dodoma ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mradi huo uliogharimu sh. milioni 700 na kuja kunufaisha zaidi watu 2000.Unatarajia kukamilika Aprili  mwaka huu. Mabomba yatasambazwa kwa umbali wa Km 23.6, uwezo wake utakuwa unatoa lita za ujazo 185,000 kwa siku.


 Wanawake wa Kijiji cha Nguji Kata ya Mundemu wakishangilia baada ya kusikia kuwa mradi huo wa maji utazinduliwa rasmi Aprili mwaka huu.
 Komredi Kinana akiendesha Trekta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa matrekta kwa ajili ya Kilimo Kwanza katika Kata ya Chonde, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akilima kwa kutumia trekta baada ya Mradi wa Matrekta ya Kilimo Kwanza kuzinduliwa na Komredi Kinana katika Kata ya Chonde, wilayani Bahi, Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni Chiku Galawa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Nguji, wilayani Bahi wakati wa ziara ya Komredi Kinana. Nyuma yake ni Katibu wake, Mwanaamani Mtoo.
 Katibu wa CCM, Wilaya ya Chamwino, Janeth akizungumza na Mhariri wa gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe (kulia) pamoja na Athuman Kido wa gazeti la Raia Tanzania wakati wa kuagana katika Kijiji cha Nguji tayari msafara wa Komredi Kinana kuanza ziara  wilayani Bahi, Dodoma.
 Kmoredi Kinana akiwapa kiti moto watumishi wa Wilaya ya Bahi kwa kitendo chao cha kutosimamia vizuri ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.






 Wananchi wakishangilia kwa furaha wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Chonde
 Komredi Kinana akishukuru baada ya kuvishwa mgolole na kupewa silaha za jadi na wazee wa Kata ya Chonde wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Bahi, Dodoma.
 Komredi Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Chonde, wilayani Bahi, Dodoma.
 Wananchi wa Kata ya Chonde wakimsikiliza kwa makini, Komredi Kinana aliyekuwa akiwahutubia.
 Komredi Kinana akimpatia kadi ya CCM mmoja wa wanachama waliojiunga na chama hicho katika Kata ya Chonde wilayani Chonde, Wilaya ya Bahi.
 Nape akikusanya mabango kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Msisi waliouzuia msafara wa  Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana ili awasaidie ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo mwaka 2011 paa ziliezuliuwa kutokana na upepo mkali uliosababishwa na mvua kuwa iliyonyesha eneo hilo.
Komredi Kinana akiendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Msingi Msisi, iliyoezuliwa na upepo mwaka 2011 na majengo hayo kuendelea kutumika hivyo hivyo na wanafunzi. Wananchi wa eneo la Msisi walizuia msafara wa Komredi Kinana wakimuomba awasaidie ujenzi wa majengo hayo ya shule. Katika Harambee yalipatikana mabati 100 na mifuko ya simenti 75 hivyo kuiagiza Halmashauri ya wilaya hiyo kuanza mara moja ujenzi ii wanafunzi wasome katika vyumba vilivyo salama.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA