17 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA AL SHABAAB

Wavamizi walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo kabla ya wavamizi kuingia wakiwa wamejihami kwa bunduki
Watu 17 wameripotiwa kuuawa na wengine 20 kujeruhiwa vibaya wakati wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shaabab waliposhambulia majengo ya wizara ya elimu mjini Mogadishu,Somalia.
Mwandishi wa BBC Mohammed Moalimu,amesema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo
Kulingana na msemaji wa idara ya usalama wa ndani Mohammed Yusuf watu 8 waliuawa na wavamizi hao huku wanajeshi wawili wakipoteza maisha yao.
Askari mmoja ni wa muungano wa majeshi ya umoja wa Afrika.
Msemaji huyo anasema kuwa wavamizi hao walikuwa ni 7 wawili waliojilipua langoni huku wengine watano wakikabiliwa na maafisa wa usalama.
Walioshuhudia wanasema wavamizi hao walitumia bomu lililotegwa ndani ya gari kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami kwa bunduki za rashasha.
Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab,
amethibitisha kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa
''wapiganaji wetu wamekwisha ingia ndani ya jengo hilo lenye wizara ya elimu''
Mapigano yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji hao kulingana na mwakilishi wa polisi.
Wapiganaji wa Al shabaab wametekeleza mashambulizi kama haya katika siku za hivi punde.
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili zilizofwatia .
Waandishi wa habari walioshuhudia matukio kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya milio ya risasi kuanza kusikika kutoka jengo hilo.
hakuna kundi lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al shabaan imekuwa ikitumia mbinu kama zilizotumika leo .
Kundi hilo la waislamu linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*