Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Adollah Mapunda akikagua timu ya netiboli wakati wa Bonanza lililoshirikisha taasisi 15 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Wachezaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), wakifurahia zawadi ya kuku waliyotwaa baada ya kuibuka kidedea katika mashindano ya kukimbiza kuku wakati wa Bonanza lililoshirikisha taasisi 15 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha
Wachezaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), wakifurahia zawadi ya kuku waliyotwaa baada ya kuibuka kidedea katika mashindano ya kukimbiza kuku wakati wa Bonanza lililoshirikisha taasisi 15 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha
Richard Mwangulube
Timu ya Soka ya chuo cha ufundi Arusha (ATC) imefnikiwa kubeba kombe la bonanza baada ya kuilipua timu ya soka ya Benki Kuu Tawi la Arusha ( BOT mabao 3-0
Ushindi huo wa timu ya ATC umekuwa faraja kubwa kwa chuo hicho kutokana na mashindano hayo yaliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa mara ya kwanza
Katika bonanza hilo timu ya soka ya Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA) ilishika nafasi ya pili
Kwa upande wa netiboli timu ya RAS Arusha ilipata ushindi mnono baada ya kuwaadhibu ndugu zao timu ya Jiji la Arusha katika mchezo wa fainali
Katika mchezo wa draft ATC wanaume imeibuka kidedea tena huku timu ya chuo cha uhasibu tawi la arusha ikishika nafasi ya pili
Kwa upande wa wanawake Halmashauri ya Arusha (Arusha DC) imefanikiwa kuinyuka timu ya chuo cha uhasibu
Kuhusu mchezo wa bao timu yaMamlaka ya Maji Arusha iliibuka na ushindi baada ya kuwacharaja vijana wa kituo cha mikutano cha kimataifa AICC kwa upande wa wanaume
Katika mchezo w akarata uhasibu wamepata ushindi huku nafasi ya pili ikichukuliwa na AICC upande wa wanaume
Katika mchezo huo wanawake Jiji Arusha wameshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na RAS Arusha
Katika kuvuta kamba wanaume chuo cha uhasibu Arusha kimeshika nafasi ya kwanza huku mshindi wa pili ikichukuliw ana chuo cha ufundi Arusha upande wa wanaume
Kwa upande wa wanawake kuvuta kamba Timu ya Jiji Arusha imefanikiw akunyakua nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliw ana Ras Arusha
Katika mchezo wa kukimbia na magunia wanaume taasisi ya utafiti TAWIRI ilishika nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikinyakuliw ana AICC
Upande wa wanawake kukimbia na magunia Uhasibu nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliw ana TAWIRI
Kuhusu mbio za watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 50 Ofisi ya RAS ilishika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na AICC upande wa wanaume
Upande wa wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa na TPRI huku nafasi ya pili ikichukuliwa na RAS ili kufanikisha bonanza hilo la kwanza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felex Ntibenda aliunda timu ya watu 18 kutoka taasisi mbalimbali
Bonanza la mwaka huku ambalo ni la kwanza taasisi zipatazo 15 zimeshikiriki katika mashindano mbalimbali ukiwemo mchezo wa kufukuza kuku
Aidha washindi wa kwanza na wa pili walizawadiwa vikombe na medali pamoja na wengine kubahatika kupata zawadi ya kuku na vyeti
Bonanza hilo lilifanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Mwisho
Comments