- Get link
- Other Apps
Sterling pichani
Raheem Sterling ameambiwa ajiheshimu kwenye mazungumzo yake na Brendan Rodgers jana siku ya Alhamisi.
Rodgers amemkumbusha Sterling wajibu wake baada ya kupigwa picha akiwa anavuta gesi ya kusisimua kucheka na akiwa pembeni na kipipa cha gesi hiyo (shisha).Rodgers anaelewa presha alionao nayo mshambuliaji huyo wa Liverpool na Uingereza na amemwambia kuwa makini.
Bosi huyo wa Liverpool pia alizungumza na kinda mwingine Jordon Ibe baada ya kinda huyo kupigwa picha akiwa na Sterling wakivuta gesi hiyo.
Ibe ndio kwanza AMERUDI kwa mara ya kwanza tokea alipumia mwezi Februari mwishoni na juzi alicheza dhidi ya Newcastle.
Comments