DC KINONDONI AKUTANA NA WANANCHI KAWE MZIMUNI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI

      

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wananchi wa Kawe Mzimuni alipofika kutatua mgogoro wa ardhi kati yao na taasisi moja ya kiislamu inayomiliki Shule ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B iliyopo eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Katibu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa eneo hilo Mgili Wambura alimwambia DC Makonda kuwa eneo hilo tangu zamani ilikuwa ni barabara hivyo wanashangaa kuvamiwa hivyo alimuomba Makonda kusaidia kuondoa mvutano huo.
 Mmoja wa wakilishi wa shule hiyo ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B,  Hamad Iddi Almas alimwambia DC Makonda (hayupo pichani), kuwa eneo hilo linamilikiwa na taasisi yao tangu siku nyingi.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, 
Paul Makonda.
Wananchi wa Kawe Mzimuni wakiwa kwenye ukuta walioubomoa kutokana na kujengwa eneo la barabara.
 …………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amezitaka pande mbili zinazogombania ardhi maeneo ya Kawe Mzimuni kufika na vielelezo vya umiliki wa eneo hilo ili kumaliza mgogoro huo.
Mwito huo ameutoa wakati akizingumza na wananchi wa eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi ambao walijichukulia sheria ya kubomoa ukuta uliojengwa na mwananchi mmoja wa eneo hilo kuwa ulijengwa kwenye barabara.
Mbali na kubomoa ukuta huo wananchi hao wanavutana  la taasisi moja ya dini ya kiislamu inayomiliki Shule ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B iliyopo eneo hilo kuwa imemega eneo la Shule ya Msingi ya Ukwamani.
“Nimekuja hapa baada ya kusikia mgogoro uliopo wa kugombea ardhi nafikiri ofisa mipango mji wa Manispaa alifika hapa kuzungumza nanyi naomba baada ya siku saba pande zote zinazovutana zije na vielelezo ofidsini kwangu hapo tutajua nani mmiliki wa eneo hilo” alisema Makonda.
Katibu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa eneo hilo Mgili Wambura alimwambia Makonda kuwa eneo hilo tangu zamani ilikuwa ni barabara hivyo wanashangaa kuvamiwa hivyo alimuomba Makonda kusaidia kuondoa mvutano huo.
Mmoja wa wakilishi wa shule hiyo ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B Hamad Iddi Almas alimwambia Makonda kuwa eneo hilo linamilikiwa na taasisi yao tangu siku nyingi jambo lililosababisha wananchi kuanza kuzomea wakipinga umiliki huo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.