Ghasia za ubaguzi zapingwa Afrika Kusini

Waandamana kupinga ghasia za kibaguzi dhidi ya wahamiaji Afrika kusini
Maelfu ya raia katika mji wa mashariki wa Durban nchini Afrika Kusini wanaandamana kupinga ghasia za hivi majuzi dhidi ya wageni.
Takriban watu watano wameuawa tangu wiki iliopita katika ghasia dhidi ya wahamiaji ambao wameshtumiwa kwa kuchukua kazi za raia wa taifa hilo.
Hofu ya kusambaa kwa ghasia inaendelea kutanda.
Raia aliyejeruhiwa kutokana na ghasia dhidi ya wageni Afrika kusini
Mjini Johannesburg ,wamiliki wa maduka kutoka mataifa ya Ethiopia,Somalia na mataifa mengine ya Afrika wamefunga biashara zao wakihofia kuporwa.
Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini ameshtumu ghasia hizo na anatarajiwa kulihutubia bunge baadaye.
Mnamo mwaka 2008 watu 62 waliuawa kufuatia ghasia za kibaguzi zilizokumba taifa hilo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI