HABARI LUKUKI KUTOKA TFF

TAREHE 14 APRILI 2015
KAMATI YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI YA BODI YA LIGI
Kocha Jackson Mayanja wa Kagera Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kutoa lugha ya kashfa kwa maneno na vitendo kwa waamuzi wa mechi yao na Mtibwa Sugar kuwa walipewa rushwa.

Adhabu dhidi ya Kocha Mayanja kwenye mechi hiyo namba 136 iliyochezwa Aprili 1, 2015 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu.

Klabu ya Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya timu yake kukataa kuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi namba 142 dhidi ya Stand United iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.  Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.

Nayo Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar. Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao.

Pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.

Kipa Tony Kavishe wa Polisi Morogoro amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mwamuzi msaidizi namba mbili, Hassan Zani kwa kuzingatia kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Alifanya kosa hilo kwenye mechi namba 147 dhidi ya Mgambo Shooting iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


KAMATI YA MASHINDANO TFF
Kamati ya Mashindano ya TFF ilikutana jana kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) pamoja na taarifa ya Ligi Daraja la Pili (SDL) iliyomalizika hivi karibuni.

Katika matukio ya SDL, Kamati imeipiga faini ya sh. 300,000 timu ya JKT Rwamkoma ya Mara kwa kusababisha mechi yake dhidi ya AFC ya Arusha kuvurugika. Adhabu hiyo kwa mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya Ligi Daraja la Pili.

Nao makocha wa JKT Rwamkoma, Hassan Makame na Kamara Kadede wamepigwa faini ya sh. 200,000 kila mmoja na kufungiwa mechi sita kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi namba moja katika mechi hiyo iliyochezwa Machi 9, 2015.

Wachezaji Shafii Maganga, Saleh Ali, Ismail Salim na Mussa Senyange wa JKT Rwamkoma ambao wanatuhumiwa kwa kushambulia mwamuzi kwenye mechi hiyo suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi.

VPL KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika viwanja viwili nchini, jijini Tanga wenyeji Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribisha timu ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba la Manungu Turiani.


TTF YAFUNGUA SEMINA YA WAAMUZI VIJANA
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine leo amefungua rasmi semina ya waamuzi vijana wenye umri wa miaka 12- 17, inayofanyika katika hostel za TFF zilizopo Karume.

Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amesema semina hiyo ya vijana imejumuisha vijana 27 kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaandaa kuwa waamuzi wa kimataifa baadae.

Vijana hawa mnaowaona hapa wanatoka katika viuto vya kufundishia waamuzi vijana nchini, wakikua na kufuata misingi ya kazi baadae watakua waamuzi bor nchini kwa sababu watakua wameanza tangu wadogo na kufuata maelekezo ya wakufunzi wao.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchin Bw. Salum Chama akiongea na wandishi wa habari kabla ya kumkaribisha katibu mkuu, amesema malengo yao ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na waamuzi wa kimataifa wengi.

Mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kutoa waamuzi 18 wenye beji za FIFA barani Afrika, nyuma ya Misri yenye waamuzi 22, Lengo ni kuhakikisha tunawaanda vijana wengi waje kuwa waamuzi wa kimataifa.

Semina hiyo ya siku 5 inatarajiwa kufungwa ijumaa tarehe  17 Mei, 2015 inajumuisha vijana kutoka mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Zanzibar, Mwanza, Arusha na Mbeya, kati ya vijana 37 waamuzi wawili ni wanawake.

Wakufunzi wa semina hiyo ni Soud Abdi, Riziki Majala na Joan Minja.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI