THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax:
255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Marekani
ni mshirika mkubwa wa Maendeleo Tanzania kwa kuunga mkono shughuli mbalimbali za maendeleo na kijamii ,
ambazo zimeleta mafanikio na mchango mkubwa katika kukuza na
kuendeleza nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jana tarehe 2 April, 2015 jijini Seattle,
katika mhadhara uliondaliwa na taasisi ya World Affairs Council na kuhudhuriwa
na wafanyabiashara , wafanyakazi wa taasisi mbalimbali walimu na
wanafunzi wa shule na vyuo kutoka Seattle.
Rais
ametoa mifano ya kazi na michango inayofanywa na Shirika la Maendeleo
ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambalo limekuwa mstari wa mbele katika
kuchangia katika misaada ya kiuchumi na kijamii, misaada ya dharura ya
kupunguza makali ya Ukimwi (PEPFER), misaada ya Milenia inayolenga
kuondoa umaskini (MCC), Mpango wa Usalama wa Chakula na Kupambana na Njaa
maarufu kama Feed the Future na Mpango wa Kusambaza umeme kwa watu wengi
zaidi barani Afrika maarufu kama Power Africa.
"Mipango na programu zote hizi
zina mchango mkubwa kwa Maendeleo ya Tanzania na Watu wake“. Rais amesema na
kuonyesha jinsi mahusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ulivyo imara
na wa manufaa makubwa.
Katika
hotuba yake, Rais Kikwete amesema anatumaini kuwa ziara yake jijini Seattle
itakuza mahusiano baina ya watu wa nchi hizi mbili na kuyafanya kukua na
kuimarika kwa kupitia uwekezaji na shughuli mbalimbali za pamoja katika sekta
za binafsi na biashara.
Rais
Kikwete yuko jijini Seattle kwa shughuli za kikazi kwa siku moja ambapo pamoja
na mambo mengine ametembelea Makao Makuu ya Taasisi ya Bill and Melinda Gates
na kufanya mazungumzo na Bw. Bill Gates.Katika mazungumzo yao, Bw. Gates
ameahidi kuendeleza juhudi zake na misaada kwa Tanzania katika sekta za Afya na
Kilimo.
"Tunatakiwa kuendeleza ushirikiano
wetu nawe kwani sauti kama yako katika masuala ya Afya na Kilimo ni
chache, hivyo tunataka kuendelea kushirikiana nawe". Bw. Bill Gates
amemwambia Rais Kikwete.
Rais
pia amefanya ziara katika Makao Makuu ya Shirika la kutengeneza ndege la Boeing
ambapo amepata maelezo na kutembelea kiwandani na kuona utengenezaji wa ndege
unaofanywa na shirika hilo.
Rais
Kikwete anaendelea na ziara katika jiji la Washington DC.
...............Mwisho...............
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari
wa Rais Msaidizi,
Seattle –Marekani.
2 April,
2015
Comments