KINANA ASHIRIKI JOGGING YA KUHAMASISHA VIJANA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiruka kutoka jukwaani wakati wa Bonanza la Klabu za Jogging la kuhamasisha Vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura eneo la Kaza Moyo, Kata ya Kipawa, Segerea Ukonga, Dar es Salaam leo, ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.
 Komredi Kinana akishiriki katika Jogging pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto), ambapo walitokea Majumba Sita hadi Jet Conner na kurudi tena hadi Mtaa wa Kaza Moyo, Segerea.
 Moja wa Klabu ya Jogging wakishiriki kwenye Bonanza hilo
 Ni mambo kwa kwenda mbele
 Ni furaha iliyoje kujenga afya kwa njia ya Jogging
 Msululu wa klabu mbalimbali za Jogging
 Nape Nauye  (kulia)akiwa jukwaani  na baadhi ya viongozi wa Klabu za Jogging 
 Komredi Kinana akishiriki mazoezi mepesi baada ya kukimbia na vijana kwa takribani KM 7

 Kinana akiangalia vijana wa jogging wakifanya mazoezi mepesi eneo la Kaya Moyo, Ukonga
 Msanii maarufu kwa jina la Saga Sumu akionesha umahiri wake kwa kuimba wimbo uliowapa hamasa vijana.
 Wasanii wa Bendi ya Ya Moto wakifanya vitu vyao  wakati bendi hiyo ilipotumbuiza Live kwenye Bonanza hilo na kukonga nyoyo za vijana kwa wazee
 Komredi Kinana akiwaonesha vijana kwamba anaweza kupiga mbinja kuliko wao.
 Katibu Mkuu wa CCM, akihutubia umati wa vijana kutoka Klabu 100 za Jogging za jijini zilizoalikwa kwenye Bonanza la kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, eneo la Kaza Moyo, Ukonga Segerea, Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)

 Nape akiungana na wanamuziki wa bendi ya ya Ya Moto kucheza wakati wa Bonanza hilo
 Komredi Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Klabu ya Jogging ya Kaza Moyo iliyoandaa bonanza hilo kwa kusaidiana na Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Karuwa (kulia) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kaza Moyo, George Mtambalike (kushoto)
Nape akizungumza na wanahabari kuhusu umuhimu wa Jogging na vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

CCM YAITAKA NEC KUTOTHUBUTU KUAHIRISHA UCHAGUZI MKUU 2015

CHAMA Cha Mapinzuzi (CCM), kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutothubutu kuahirisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho tawala, Nape Nnauye, wakati wa Bonanza maalumu la Klabu za Jogging la kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili wapate fursa ya kupiga kura.

Nape, alitoa rai hiyo, eneo la Kaza Roho, Ukonga, Dar es Salaam jana, baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo wa chama hicho kuhusu fununu zilizopo kwamba kuna mpango wa kuahirisha uchaguzi Mkuu. 

"Wenye wajibu wa kupanga masuala ya Uchaguzi Mkuu ni NEC, lakini mimi nawashauri wasithubutu kuahirisha, ufanyike kama ilivyo kawaida mwezi wa Oktoba, ili wananchi wapate haki hayo ya msingi kuwachagua viongozi wanaowataka,"alisema Nape.

Pia, aliitaka NEC, kuwaandalia utaratibu mzuri vijana kwa kuanzisha dawati maalumu la kuwaandikisha  katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kuondoa baadhi ya maswali yasiyo ya msingi yanayowakatisha tamaa.

Vilevile, Nape alitoa wito kwa vijana nchini kuacha ushabiki na itikadi za kisiasa, bali wajitokeze kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari hilo ili wapate haki yao ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka. 

Mgeni rasmi katika Bonanza hilo lililoshirikisha zaidi ya vikundi vya Joging 100 vilivyoalikwa kutoka wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala, Dar es Salaam, Alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Viongozi wengine walioshiriki kwenye bonanza hilo lililoandaliwa na Klabu ya Joging ya Kaza Moyo cha Ukonga Segerea,ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, Mbunge wa Jimbo la Segerea, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga pamoja na viongozi waandamizi wa CCM, Mkoa wa mkoa huo.

Komredi Kinana aliongoza Mbio za Bonanza hilo kutoka Majumba Sita hadi Jeti na kurudi tena kwenye barabara ya Nyerere hadi Uwanja wa uliopo Mtaa wa Kaza Moyo, Kata ya Kipawa, Ukonga. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA