KITWANGA AFAGILIA MGODI WA BUZWAGI


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uchimbaji Madini, Acacia, Brad Gordon, (kushoto), wakiongozwa na Meneja Mkuu wa Mgodi wa kuchimba dhahabu wa Buzwagi, wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, ambaye ni mtanzania, Filbert Rweyemamu, kutembelea eneo la uchimbaji wa wazi (open pit), Jumamosi jioni . Naibu waziri huyo pia alitembelea na kujione jinsi mgodi wa Buzwagi unavyovuna na kuhifadhi maji. Naibu waziri Kitwanga, ameisifu kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi, kwa mpango wake wa kuwapatia mafunzo ya kiuongozi na kurithisha,(Succession plan),  uongozi wa juu kutoka kwa wataalamu kutoka, nje, (Expertts) na kuwapa watanzania. Mgodi wa Buzwagi unaongozwa na Mtanzania Filbert Rweyemamu, na Bulyanhulu amekuwa akikaimu Mtanzania Benedict Busunzu, wakati meneja mkuu wake, Michel Ash anapokuwa hayupo

Naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, (wakwanza kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Brad Gordon, (wapili kulia), makamu wa rais wa kampuni hiyo anayeshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, (katikati), na viongozi wengine wa mgodi huo na wa wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wakitembelea eneo la uchimbaji madini la wazi mgodi wa Buzwagi,  mwishoni mwa wiki. Buzwagi water reserve pond

Makamu wa rais wa kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, anayeshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, (kushoto), akiteta jambo na Meneja wa ustawi wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo, wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya kiutendaji ya mgodi wa Buzwagi, kilichofanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili Aprili 12, 2015

Brad akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, wakati akipokea taarifa ya kila mwezi ya utendaji kazi kwa kila idara ya mgodi huo

Mkuu wa kitengo cha usalama mgodi wa Buzwagi, wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, ACP, Jamal Rwambo, akitoa ripoti ya hali ya usalama wa mgodi na wafanyakazi wa mgodi huo, katika kipindi cha mwezi uliopita, ambapo alisema, hakuna tukio lolote la tishio au usalama imam wa mgodi au mfanyakazi yeyote, lililotokea.

Meneja Mkuu wa Mgodiwa Buzwagi, ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Filbert Rweyemamu, akiokota kadi wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya wafanyakazi waliofanya vizuri katika kipindi cha mwezi uliopita, wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya kiutendaji ya kila idara ya mgodi huo usiku wa kuamkia leo Jumapili Aprili 12, 2015

Meneja wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa umma, wa kampuni ya Acacia, Necta P. Foya, (kulia), na mkuu wa kitengo wa usalama mgodi wa Buzwagi, ACP, Jamali Rwambo, na wafanyakazi wengine, wakifuatilia taarifa ya mgodi wa Buzwagi, iliyokuwea ikitolewa na Meenja Mkuu wake, Filbert Rweyemamu, kwa naibu waziri wa nishati na madini, Charles MKitwanga, alipotembelea Jumamosi alasiri, Aprili 11, 2015

Malori makubwa, yakisomba mchanga uliochimbwa kwenye eneo la mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, wakati wa ziara ya naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, Jumamosi jioni Aprili 11, 2015

Sehemu ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, waliohudhuria kikao cha kila mwezi cha kupokea ripoti ya kiutendaji

Sehemu ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, waliohudhuria kikao cha kila mwezi cha kupokea ripoti ya kiutendaji

Sehemu ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, waliohudhuria kikao cha kila mwezi cha kupokea ripoti ya kiutendaji

Sehemu ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, waliohudhuria kikao cha kila mwezi cha kupokea ripoti ya kiutendaji 
Rwambo (kushoto), akimnong'oneza jambo Meneja Mkuu Rweyemamu

Afisa Madini Mkazi, wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Sopha Omary, (kushoto), akizungumza njambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (kulia), na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu

Naibu waziri Kitwanga, (katikati), akipewa maelezo ya uvunaji na utunzaji maji na mtaalamu wa mazingira wa mgodi wa Buzwagi, wakati wa ziara hiyo. Kulia ni Meneja Mkuu, Filbert Rweyemamu

Makamu wa rais wa Acacia, anayeshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, (kulia), akitoa shukrani kwa niaba ya kampuni hiyo, mwishoni mwa ziara ya naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, (katuikati), aliyoifanya kwenye migodi ya Bulyanhulu wilayani Msalala, na Buzwagi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, Jumamosi Aprili 11, 2015. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu, wa Acacia, Brad Gordon




Naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, akiwaeleza waandishi wan habari, baada ya kutembelea migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi iliyoko mkoani Shinyanga

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA