Mbunge wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa akishiriki kucheza kwaito na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda leo |
Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda akimpongeza mwalimu wa kujitolea wa Hesabu Shuleni hapo mbele ya mbunge Godfrey Mgimwa |
Mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa kushoto akikavbidhi zawadi kwa walimu wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda |
Wanafumnzi wa kidato cha sita wakikabidhiwa vyeti na mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa |
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda wakimpokea mbunge wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa kwa gwalide maalum |
Mbunge Mgimwa wa tatu kulia akiongozana na mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Abed Kiponza kulia na viongozi mbali mbali wa shule hiyo ya serikali ya kijiji cha Ifunda |
Mbunge Mgimwa akivishwa skafu |
Mbunge Mgimwa akitazama mwanafunzi wa Ifunda akimpasua Simbilisi |
Baada ya upasuaji kufanyika |
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari ya wasichana Ifunda Abed Kiponza akimpongeza mbunge Mgimwa |
Mbunge Mgimwa akiwahutubia wanafunzi na wazazi |
Na MatukiodaimaBLOg
BAADA ya wanafunzi kukosa darasa kubwa la kusomea ,mbunge
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa amejitolea kuanza ujenzi wa darasa hilo kuahidi kuchangia mifuko
200 ya Saruji yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 3 kwa ajili
ya kusaidia ujenzi wa darala litakalotumiwa na wanafunzi
zaidi ya 200 katika shule ya sekondari ya wasichana Ifunda katika
wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Mbunge
Mgimwa ambae alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 9 ya
shule hiyo ametoa ahadi leo kufuatia maombi ya uongozi wa
shule hiyo .
Alisema
kuwa lengo lake kuona kiwango cha elimu katika jimbo lake
kinaendelea kukua zaidi na ndio sababu ameendelea kusaidia
ujenzi wa maabara pamoja na kuchangia shughuli mbali mbali za
kimaendeleo zinazofanywa na wananchi wake zikiwemo za ujenzi wa
shule ,nyumba za walimu pamoja na ujenzi wa maabara zinazojengwa
kufuatia agiza la Rais Dkt Jakaya Kikwete.
"Leo
hapa nimeelezwa changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hii
kwanza juu ya uchakavu wa majengo ,uhaba wa walimu wa masomo ya
Hisabati na Sayansi lakini pia ukosefu wa darasa kubwa
litakaloweza kuchukua wanafunzi 200 kwa wakati mmoja na mmeomba
kusaidiwa kati ya bati 200 ama Saruji .......sasa ili ujenzi
huu uanze mimi nitachangia saruji mifuko yote 200 ila rai yangu
kwa wazazi tuungane katika ujenzi huu"
Kuhusu
tatizo la uhaba wa walimu alisema kuwa hiyo ni changamoto ya
nchi nzima japo alisema lazima atalifikisha kwa mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa ili kuweza
kuitazama shule hiyo kwa jicho la tatu .
Pia
mbunge huyo alisema kuwa toka ameingia madarakani mwaka jana
kuna baadhi ya kazi kubwa amepata kuzifanya katika jimbo hilo na
kuwa wananchi wa jimbo hilo ni mashahidi katika suala hilo na
kuwa akiwa kama mwakilishi wa wananchi wa Kalenga atahakikisha kwa
muda uliobaki kuona anatafuta majibu ya changamoto mbali mbali za
jimbo hilo.
Aidha
mbunge huyo aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kazi nzuri ya
ukuzaji wa taaluma shuleni hapo na hata kuifanya shule hiyo kuwa
moja kati ya shule zenye sifa nzuri ya kufaulisha ndani ya wilaya
ya Iringa ,mkoa na taifa na kuwataka wahitimu wa kidato cha
sita kutumia muda uliobaki kujisomea zaidi ili kuendeleza rekodi
ya kufaulu vema katika mitihani ya kidato cha sita.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule hiyo Abed Kiponza akimshukuru mbunge Mgimwa
alisema kuwa msaada huo ni ukombozi mkubwa wa maendeleo ya ujenzi
wa darasa hilo pia aliwaomba wazazi na wadau mbali mbali
kujitolea kushiriki ujenzi wa darasa hilo pamoja na uboreshaji wa
majengo ya shule hiyo .
Kiponza
alisema kuwa shule hiyo ni shule ambayo imekuwa ikiendeshwa
kwa misingi bora ya kitaaluma na kuwa haijapata kuwa na mgomo wa
wanafunzi wala walimu tofauti na shule nyingine .
Mkuu
wa shule hiyo Bi Zaina Salingwa katika taarifa yake kwa wazazi
na mgeni rasmi alisema kuwa shule hiyo ilianza mwaka 2005 baada
ya kufungwa kwa kilichokuwa chuo cha ualimu Ifunda na kuwa hali
ya majengo hayo ni chakavu zaidi baada ya majengo hayo kujengwa
toka mwaka 1985.
Alisema
kuwa shule hiyo ni shule ya bweni yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 640 lakini ina wanafunzi 653 wakiwepo wanafunzi 440 wa
kidato cha tano na wanafunzi 213 wa kidato cha sita na kuwa asilimia 90
ya wanafunzi wanasoma masomo ya Sayansi na jumla ya michepuo
waliyonayo ni saba yani CBG, PCB, PCM, PGM,EGM,HGK na HGE na kuwa
walimu waliopo ni 23 huku masomo ya Sayansi na Hesabu yakiwa
hayana mwalimu hata mmoja zaidi ya kukodi walimu kutoka nje.
Mkuu
huyo alisema kuwa hadi sasa shule hiyo imefanikiwa kuwa na gari
la mkuu wa shule ambalo limenunuliwa kwa kiasi cha Tsh milioni
20 fedha zilizochangwa na wadau mbali mbali akiwemo kamanda wa
UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas .
Comments