Polisi watumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu Iringa mjini

 Askari  wa  FFU  wakiwa katika  eneo la Ipogolo  mjini Iringa  kutuliza vurugu za wananchi waliokuwa  wakichoma mataili barabarani  kufuatia  mtoto  mmoja kugongwa na gari na kufa (pichamatukiodaimaBlog )


  Askari  wa FFU  wakiendesha  msako  kwa  vijana waliohusika na vurugu hizo

  Askari  wa FFU  Iringa  wakipita   kando ya moto  wa mataili  uliochomwa katikati ya barabara ya  Iringa - Kilolo  eneo la stendi la Ipogolo jana  baada  ya  mtoto  kugongwa na  gari na kufa (picha na matukiodaimaBlog )

Askari  wa  kikosi cha Zimamoto mjini Iringa ambae jina lake  halikuweza  kufahamika akipongezwa na mmoja kati ya  wazee  walikuwa  wakikimbia mabomu na kujificha chini ya mtaro  wa maji (picha na matukiodaimaBlog)

VURUGU  kubwa  zimetokea leo   katika  eneo la Ipogolo  mjini Iringa na  kupelekea askari wa   kikosi cha kutuliza  ghasia  (FFU)  kutumia  mabomu ya machozi  kuthibiti vurugu    baada ya mtoto wa  miaka kata 6 kugongwa na gari  wakati  akifanya biashara ya  kuuza mbogo mboga .


  Wananchi wanaosadikika  kuwa na  hasira kali  walianza kuwashambulia  askari  polisi waliofika kuchukua mwili huo kwa mawe  kwa madai ya  kuchelewa  kufika  eneo la  tukio.

Wakizungumzia  tukio   hilo kwa mwandishi wa habari hizi  baadhi ya  wananchi   walisema  kuwa  mtoto   huyo  aligongwa  majira ya saa 7 mchana na zaidi ya saa  moja baada ya  kutoa taarifa  polisi  ndipo  walipofika  eneo la  tukio jambo lililowakwaza  wananchi hao .


Walisema  kuwa  mbali ya  polisi  hao  kufika  pia tayari  baadhi ya askari  waliopo eneo hilo la stendi kuu ya Ipogolo  kwa  kushirikiana na  wananchi  walifanikiwa  kulikamata  gari  ambalo  lilisababisha ajali  hiyo .


Alisema  Neema Sanga  kuwa wakati  tukio  la kugongwa  mtoto  huyo  likitokea  alikuwa jirani na eneo hilo katika  msiba  na kuwa  wakati  akiwa ameingia ndani ya nyumba  hiyo  yenye msiba  kusaidia  kugawa  chakula ghafla  alipata taarifa  kuwa wananchi  wameanza vurugu kwa  kuchoma  moto matali katika barabara  hiyo  kuu ya  Iringa- Kilolo.

Hata   hivyo  alisema  kuwa  tukio  hilo  lilichukua  zaidi ya dakika 45  polisi  hao wa FFU  kufika na kuanza  kutuliza  vurugu  hizo kwa  kupiga mabomu ya machozi  kuwatawanya  wananchi zaidi ya 500  waliokuwa  wamekusanyika eneo hilo kuzuia  magari  kuendelea kupita katika  barabara  hiyo  huku  baadhi yao  wakitaka  kufunga  barabara  kuu ya  Mbeya  - Iringa ambayo haihusiki ka bisa na   eneo  lililotokea  tukio hilo.

" Ni  kweli  mtoto kagongwa na gari na kufa  tukio ambalo ni kusikitisha sana na  polisi baada ya  kupigiwa simu  wamefika  eneo la  tukio na  kuchukua maiti ya  mtoto  huyo lakini  tunajiuliza kwanini  vijana hao kuanza  kuwapiga mawe  polisi na kufanya  vurugu  wakati gari  lililogonga mtoto huyo  likiwa  limekamatwa .."  alihoji Bi  sanga

 Kuwa kwa  upande  wake hakuona  sababu za  polisi  kupigwa  wala  wananchi hao kuchoma moto  barabara wakati ajali  hiyo kama ajali nyingine na tayari  gari  lililosababisha ajali  likiwa  limekamatwa .

Bi  Sanga  alisema  wakati  mwingine  polisi  wanalalamikiwa kuwa wanatumia  nguvu  zaidi  ila kwa  tukio   hilo lawama  zake anazipeleka kwa  wananchi wenzake ambao walionyesha  kufanya vurugu kwa kuchomo moto  barabara  hiyo ya lami na   kupiga  polisi huku  wakitambua  wazi  polisi si  waliosababisha ajali  hiyo.


 Huku kwa  upande  wake mmoja  John Kalinga  akiomba  serikali kupitia  wizara ya miundo  mbinu  kuangalia   uwezekano  wa  kuweka matuta katika eneo hilo kwa madai kuwa  hii ni ajali ya  pili  kutokea na kusababisha  vifo  toka  eneo hilo  lilipowekwa  lami .

Mwandishi  wa habari hizi  alishuhudia baadhi ya  vijana  wakikimbilia kujificha katika nyumba  moja  iliyopo eneo hilo ambayo  ilikuwa na msiba   huku baadhi yao  wakijifungia  katika maduka  na bar  zilizopo eneo hilo kabla ya  polisi  kuwafuata na  kuwakamata   huko  walikojificha na  kuwaacha   wale  waliokimbilia msibani .

Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi hakuweza  kupatikana  kuzungumzia tukio  hilo  huku idadi ya vijana  waliokamatwa  kwa tuhuma za  kuhusika katika  vurugu  hizo zaidi ya 20  walionekana  wakipagiwa katika magari  ya  polisi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*