THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa furaha na unyenyekevu uteuzi iliofanywa na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Ban Ki Moon kuwa Mwenyekiti wa Jopo la
Ngazi ya Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Afya (High - Level
Panel on Global Responses to Health Crises) .
"Ni
majukumu makubwa na yenye changamoto nyingi lakini dunia inahitaji tuwe
na mikakati katika masula haya ambayo ni muhimu kwa maisha ya binadamu, hivyo
hatuna budi kufanya kazi hii Kama mchango wetu kwa ajili ya maisha ya wanadamu
na dunia kwa ujumla". Rais amesema mara
baada ya kutolewa kwa Tangazo hilo tarehe 2 April, 2015.
Wengine
walioteuliwa katika Jopo hili ni Bw. Delos Luiz Nunes Amorim wa Brazil, Bi.
Micheline Calmy-Rey wa Switzerland , Bw. Marty Natalegawa wa Indonesia, Bi. Joy
Phumaphi wa Botswana na Bw. Rajiv Shah wa Marekani.
Jopo
linatarajiwa kufanya kikao chake cha kwanza mapema Mwezi Mei, 2015 na
linatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu Mkuu wa UN mwishoni mwa Mwezi
Disemba, 2015.
.........Mwisho……….
Imetolewa na;
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Seattle - Marekani
3 Aprili, 2015
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Seattle - Marekani
3 Aprili, 2015
Comments