WIZARA YA AFYA YARIDHISHWA NA VIWANGO TBL

 Mshauri wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Phocus Lasway akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe (kulia) wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
 Meneja Mdhibiti Viwango wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Conchesta Ngaiza (kulia) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa nVipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
 Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Calvin Martin akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
 Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Calvin Martin (kulia) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye koti) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali a wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na watumishi wa wizara hiyo baada ya ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeonesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa bia zake.Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri  wa Wizara hiyo Dk Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa wizara yake kutembelea maeneo yaliyo katika utaratibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

“Hapa TBL tumegundua kuna uwelewa  wa hali ya juu kwa watumishi, wafanyakazi, wasimamizi na menejimenti  ya kampuni hii kwa kweli viwango ni vizuri na hasa katika ufuatiliaji wa wa afya za wafanyakazi,” alisema na kuongeza kuwa walijionea uzalishaji wa bia mbalimbali kiwandani hapo kwenye chupa na kadhalika.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, malengo mwaka huu ni kufanya usimamizi katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma kwa wananchi kama viwanda na kuogeza ni lazima viwanda viendane na viwango vinavyotakikana kisheria na kimataifa na kwamba wizara yake sasa hivi haikai na kusubiri ripoti za mezani bali wanatembelea maeneo yaliyo chini yao ili kujihakikishia kuhusu suala la viwango.

 Naibu Waziri huyo, ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali kutoka wizarani na Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA), aliwapongeza viongozi wa TBL kwa kujipanga vizuri  katika utendaji  wao.

“Tumetembelea viwanda mbalimbali lakini hapa mmejipanga vizuri zaidi, alisema baada ya kupokea
maelezo mbalimbali kutoka kwa viongozi wa TBL waliokuwepo kwenye ziara hiyo.

Dk. Kebwe pia aliipongeza TBL kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwajali wafanyakazi kwa kuanzisha Programu ya Ukimwi katika sehemu ya kazi ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kuhamasisha upimaji wa mara kwa mara na pia kuhumiza matumizi ya kinga dhidi ya ugonjwa huo.

Katika maelezo ya utangulizi, Naibu waziri huyo alielezwa kuwa TBL ina utaratibu wa kupima wafanyakazi wake mara moja kwa mwaka na kwa kipindi cha kuanzia Aprli mwaka jana hado Machi mwaka huu zaidi ya asilimia 83 ya wafanyakazi walipima afya yao kuona kama wameathirika au la.

“Hii ni dalili nzuri sana na nawapongeza kwa hatua hii na ni matumaini yangu kuwa kuanzia sasa na kuendelea mtaanza kupima mara mbili kwa mwaka nivyo sheria inavyotaka,” alisema.Meneja wa Kiwanda Cha Dar es Salaam, Calvin Martin, alisema wamefarajika mno kwa ujio huo wa Naibu Waziri ili aweze kujionea namna kampuni hiyo imekuwa ikizingatia suala la viwango katika uzalishaji wake.

“Tumewaonesha maeneo yote na wameonesha kuridhishwa na viwango na haua ambazo bidhaa zetu zinapitia kabla ya kwenda kwa mlaji,” alisema na kuongeza kuwa wana nia ya kuendelea kuboresha viwango vyao ili kampuni hiyo iendelee kuwa bora zaidi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI