ADEBAYOR 'AIANIKA' FAMILIA YAKE....AMUUMBUA HADI MAMA YAKE MPENDA FEDHA KULIKO UTU, ASEMA...
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Adebayor amefunguka kwenye akaunti yake ya Facebook, akielezea kila kitu ambacho amefanya kwa ajili ya ndugu zake na mama yake.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye amekanusha taarifa za kumfukuza mama yake knyumbani kwake Novemba, aliorodhesha kila kitu alichowanunulia familia yake na ndugu zake wakati wa soka lake la kilipwa.
Adebayor amesisitiza kwamba ameamua kuujulisha uma juu ya malumbano na familia yake ili kuzisaidia familia zingine za Afrika kujifunza kutoka kwenye familia yake.
Emmanuel Adebayor ameweka picha hii Facebook sambamba na taarifa ya maneno 877
Mshambuliaji wa Tottenham, Adebayor amekanusha kumfukzua mama yake Novemba mwaka jana
Mchezaji huyo wa Togo, ambaye alirudishwa katika katika kikosi cha kwanza cha Tottenham dhidi ya Manchester City, Jumapili iliyopita baada ya kukaa benchi kwa miezi miwili, alitumia maneno 877 kuelezea jambo hilo.
Alieleza jinsi alivyolipa kwa ajili ya mama yake kwenda kufanyiwa vipimo London, pia kumuacha dada yake kukaa kwenye nyumba ya dola milioni 1.2 iliyopo nchini Ghana na kumsaidia mmoja wa kaka zake kuanzisha biashara, pamoja na kuwalipia watoto wa kaka yake huyo ada ya shule.
Nyota wa Ligi Kuu England, Adebayor (kulia) hivi karibuni amerejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu
Adebayor, ambaye alihamia England mwaka 2006 baada ya kusajiliwa na mahasimu wa Tottenham, Arsenal, alisema pia alimpeleka mama yake kwa mchungaji wa Nigeria, T. B. Joshua akae wiki kadhaa, lakini aliondoka baada ya siku mbili.
Pia mshambuliaji huyo wa Ligi Kuu England alikosolewa kuhusu marehemu kaka yake Peter, lakini alifunguka kwamba hakuruhusiwa kumuona kaka yake alipokuwa anaumwa na kuambiwa atoe fedha kwa ajili yake.
Mchezaji ambaye alikutana na mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba kujadiliana matatizo yake, aliongeza kwamba alianzisha mfuko wa hisani Afrika kabla hajafa.
Katika maelezo mbalimbali aliyoweka kwenye mtandao wa Facebook, Adebayor alisema: “Watu wengi wamenishauri kufuata ushauri kwa kutoka kwa Drogba.
“Nilikaa chini na Drogba na ushauri mkubwa aliyonipa ni kufanya kile ambacho kitaniridhisha na kuwa na furaha. Pia niwashauri ndugu zangu Kola Adebayor, Roten De Lux Adebayor na dada yangu Lucia Adebayor wakatafute kazi za kufanya.'
Alifikiria kwamba anahitaji kwenda redio ya Peace FM, Novemba mwaka jana kukanusha maneno ya dada yake Maggie kwamba alimfukuza mama yake kwenye nyumba.
Dada yake Margaret katika mahojiano marefu na redio hiyo ya Peace FM, alidai kwamba sababu ya mchezjai kumfukuza mama take kwenye nyumba hiyo ni kwa kuwa alidhania ni mchawi, lakini mwenye Adebayor, alisema: “Sijamfukuza mama. Aliamua kuondoka mwenyewe.
“Nitakuwaje karibu na mama yangu kama yeye anawaambia watu kwamba mambo yangu hayatakuwa mazuri, hivyo nitaendelea kufanya mambo yangu.”
“Wanatakiwa waache kuchonga, wanatakiwa waache kunifanyia uchawi, waniache mwenyewe. Nilinunua nyumba ya dola milioni 1.2 (shilingi bilioni 2.3) iliyopo eneo ya East Legon kwa huyo anaechonga na kujiita dada yangu. Unaweza kuamini huyo dada ameenda kupangisha nyumba hiyo bila ya kunijulisha?'
Haijakuwa wazi kwamba nani alikuwa anamwambia aache kumfanyia ushirikina mchezaji huyo.
Adebayor hivi karibuni alizungumza na mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba juu ya matatizo yake binafsi
Maisha yake; Adebayor, ambaye jina lake kamili ni Sheyi Emmanuel Adebayor, alizaliwa mjini Lome nchini Togo, Februari 26 mwaka 1984.
Mchezaji huyo ambaye wazazi wake ni watu wa jamii ya Yoruba, alikuwa akiichezea klabu yake ya kwanza ya Sporting Club de Lome na kuonekana na wakala wa Metz, ambaye alimchukua kwenda nae Ufaransa mwaka 1999.
Nyota huyo wa Tottenham Hotspur na Togo, amezichezea klabu za Metz, Monaco, Arsenal, Real Madrid na Manchester City.
Adebayor, ambaye ni mkristo ameoa na ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Kendra, aliyezaliwa Juni mwaka 2010.
Akizungumzia kuhusiana na imani yake, Adebayor, alisema: “Kila ninachofanya katika maisha yangu nayawekaa kwenye mikono ya Mungu, muumbaji wangu. Amenipa nafasi ya kuwepo pale nilipo mimi na ndiye anaeweza kuchukua kile nilichonacho. Hakuna kitu muhimu kwangu zaidi ya Mungu." Adebayor hakuweza kutembea kwa miaka minne katika maisha yake. Mama yake alimzungusha Adebayor kila sehemu kutafuta tiba.
Mwenyewe alizungumzia mkasa huo na kusema: “Nilikuwa kanisani nikiwa nimelala chini, ilikuwa Jumapili saa 3:00 au 4:00 asubuhi, nilikuwa nikisikia watoto wakicheza nje. Ghafla kuna mmoja akaupiga mpira ndani ya kanisa. Mtu wa kwanza kusimama na kukimbia nilikuwa ni mimi, kwasababu nilikuwa nataka kuupata ule mpira.” Kuanzia hapo mchezaji huyo alinza kutembea baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa miaka minne.
Comments