Na Berthar Lumala
TAIFA
Stars imeaga rasmi michuano ya Cosafa baada ya leo kukubali kichapo cha
mabao 2-0 dhidi ya Mdagascar kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng jijini
Rustenburg, Afrika Kusini.
Kipigo
hicho kimeendeleza rekodi mbaya ya Nooij ambaye tangu aanze kuinoa Stars
ikiwa ni mechi ya 15 , ameshinda tatu, sare sita na vipigo sita.
Nooij alirithi mikoba ya Mdenmark Kim Poulsen aliyetimuliwa bila sababu za msingi.Baada
ya mechi hiyo kumalizika, Nooij amesema: "Kikubwa si matokeo, tunaandaa
timu ya kuikabili Uganda katika michuano ya CHAN na Misri katika
mashindano ya AFCON.(P.T)Matokeo
hayo yameifanya Madagascar kufikisha pointi sita baada ya kushinda 2-1
dhidi ya Lesotho katika mechi ya kwanza ya Kundi B iliyochezwa Jumatatu
wakati Stars ililala 1-0 dhidi ya Swaziland.
Madagascar
walienda mapumziko wakiongoza kwa mabao mawili yaliyofungwa na winga wa
kushoto Njiva Rakotoarimalala na mshabuliaji Rhino Randriamamaka.
Bao la
kwanza limetokana na shambulizi la kushtukiza winga huyo alipotumia
fursa ya makosa ya kujisahau na kujichanganya kwa mabeki wa Stars
waliompa nafasi mfungaji kutuliza mpira kisha kumtungua kwa shuti kali
la mguu wa kulia kipa Deogratius Munishi 'Dida' katika dakika ya 13.
Randriamamaka
akafuta ndoto za Watanzania kushinda baada ya kufumua shuti kali la
mguu wa kulia lililobabatiza vidole vya Dida akimalizia kwa ufundi kazi
nzuri ya mfungaji wa bao la kwanza, Rakotoarimalala ambaye aliwapiga
chenga mabeki wa Stars na kupenyeza pasi ya kisigino kwa mshambuliaji
huyo.
Kipindi
cha pili kocha wa Stars, Mart Nooij, aliwatoa winga Mrisho Ngasa,
mshambuiliaji Juma Liuzio na kiungo Said Ndemla kisha nafasi zao
kuchukuliwa na winga Simon Msuva, beki Shomari Kapombe na mshambuliaji
Ibrahim Ajibu, mabadiliko ambayo hayakuisaidia timu yake kupata bao hata
moja dhidi ya timu hiyo iliyopo nafasi ya 150 katika viwango vya FIFA
kwa sasa.
Kikosi
cha Taifa Stars kilianza na Deogratius Munishi, Erasto Nyoni, Oscar
Joshua, Aggrey Morris, Salum Mbonde, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar,
Said Hamis Ndemla/ Shomari Kapombe, John Bocco, Juma Luizio/ Ibrahim
Ajibu na Mrisho Ngassa/ Simon Msuva (dk 46).
Comments