FLAVIANA MATATA AONGOZA MAMIA YA WANAMITINDO WA BONGO KUJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF



Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ambaye ni Mwanamitindo na Mbunifu Mavazi maarufu nchini Tanzania,  kwa sasa akifanyia kazi zake nchini Marekani, akizungumza wakati wa semina ya siku moja, iliyowaleta pamoja, wanamitindo "kinda" wa Tanzania, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Jumapili Mei 17, 2015. 

Semina hiyo ililenga kuwafunza na kubadilishana uzoefu juu ya tasnia hiyo inayokuwa kwa kasi. Semina hiyo ya siku moja, ilitayarishwa kwa pamoja na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na mwanamitindo huyo nguli. Katika maelezo yake, Flaviana,  alisema yeye binafsi ni mwanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa hiari yaani "PSPF Supplementary Scheme-kwa kifupi PSS", na kuwataka wanamitindo waliohudhuria semina hiyo, kufuata nyayo zake. 

Aliwaeleza umuhimu wa wanamitindo hao ambao wengi ni vijana, kujiunga na mpango huo kwa faida yao ya sasa na baadaye, kwani yeye anafaidika sana kuwa mwanachama wa Mfuko huo. Baada ya maelezo hayo yaliyofuatiwa na balozi mwingine wa Mfuko huo, Msanii maarufu wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, naye aliwapa "doze" wanamitindo hao juu ya ukuhimu wa wao kuchangamkia fursa mapema kwani ndio mtindo wa kisasa. 

Hali kadhalika afisa masoko wa Mfuko huo Magira Werema, aliwahakikishia wanamitindo hao kuwa Mfuko huo ni Mfuko bora na wala hawatajuta waingiapo kuwa wanachama. Baada ya hotuba hizo, wanamitindo hao walizichangamkia fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko huo amba;po karibu washiriki wote zaidi ya 100 walijiunga na Mfuko huo.
Wanamitindo wakiwa kwenye foleni ya kupiga picha tayari kujipatia vitambulisho baada ya kukamilisha zoezi la kujaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS wa Mfuko huo.
Wanamitindo wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magira Werema, akitoa maelezo ya kina kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na Mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akizungumza jambo na wenzake, Magira Werema, (kushoto), na Colleta Mnyamani, ambaye ni Afisa Uhusiano wa Mfuko huo.
Flaviana (kulia) na Zuli Remtula,(katikati),  mwanamitindo mwingine nguli nzhini,na washiriki wengine wa semina hiyo, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Afisa wa PSPF, Magira Werema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*