HABARI MPASUKOOO!!!!!!!!! MAJAMBAZI YAMPORA MUASIA MAMILIONI YA SHILINGI DAR

Dereva na raia mwenye asili ya kiasia wakiwasiliana kwa simu na watu wao wa karibu sekunde chache baada ya majambazi kuwapora kiasi cha fedha kisichojulikana mchana majira ya saa 6 karibu na mataa ya Chang'ombe, Dar es Salaam. PICHA, HABARI  NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

MAJAMBAZI wamempora raia mwenye asili ya kiasia kiasi cha fedha kisijoulikana baada ya kumtishia kwa bastola akiwa kwenye gari dogo karibu na mataa ya Chang'ombe, Dar es Salaam.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wa habari hizi, aliyekuwa kwenye daladala, lilitokea majira ya saa 6 mchana wa leo, ambapo majambazi hao wawili waliokuwa kwenye pikipiki aina ya Discover waliteremka haraka na mmoja wao mwenye bastola alitoa na kuwatishia waliokuwa kwenye gari kwa kuwaamuru kuwapatia haraka fedha.

Wakati jambazi mwenye siraha akitishia hivyo kupitia dirisha la dereva, mwingine asiyekuwa na silaha alikuwa dirisha alilokuwa amekaa raia huyo mwenye asili ya kiasia, ambaye baada ya kuona hivyo alitoa furushi lenye fedha na kumkabidhi haraka jambazi huyo.

Tukio hilo lilichukua takribani dakika tatu, ambapo baada ya kufanikiwa waendesha pikipiki walikaribia na kuwachukua majambazi hao na kutokomea kuelekea upande wa Tazara.

Asilimia kubwa ya abiria waliokuwa ndani ya daladala na magari mwengine yaliyokuwa karibu na tukio hilo waliogopa na wengi wao waliamua kujinusuru kwa kuinama chini li wasidhurike.

Hadi tunaondoka hapo hakuna polisi yeyote aliyekuwa amefika kwa ajili ya upepelezi zaidi wa tukio hilo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.