HATIMAYE MGOMO WA MADEREVA WA MABASI UMEKWISHA, MABASI YAMEANZA KUSAFIRI LEO MCHANA

Hatimaye mgomo wa madereva wa mabasi  ulioingia siku ya pili, umemalizika baada leo mchana madareva kukubali kurudi kuendesha tayari kwa safari za kwenda mikoani kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, Dar es Salaam kuanzia saa 7 mchana.

Madereva hao inadaiwa wamekubali baada ya serikali kusikiliza kilio chao na kuahidi  kukifanyia ufumbuzi wa haraka. Pia Waziri Mkuu ameunda Tume ya Watu 13 ya kushughulikia matatizo ya madereva wa mabasi, Daladala na malori nchini.

Pia mazungumzo ya madereva na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda na Waziri Mkuu Kivuli, Freeman Mbowe walikwenda na kufanya nao mazungumza yaliyochangia kuwashawishi madareva hao kuanza tena safari.

Habari zilizotufikia punde kutoka mikoani ni kwamba tayari nako mgomo umeisha  na mabasi yameanza safari kwenda mikoa mbalimbali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI