HIFADHI YA MLIMA KILIMANJARO YATANGAZA OFA YA KUPANDA MLIMA


Mhifadhi utalii katka hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Eva Mallya akizungumza juu ya ofa iliyotangazwa na hifadhi hiyo ya kupanda mlima huo kwa siku moja na kurudi hadi kilele cha Shira.

Afisa masoko wa KINAPA ,Antypas Mgungusi akisistiza jambo wakati akizungumzia juu ya ofa ya safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro huku akishauri wenye sherehe zao kutumia nafasi hiyo kupanda Mlima huo kwa ajili ya kufanya sherehe zao,alitaja sherehe ambazo zinaweza fanyika katika hifadhi hiyo ni pamoja na wale wenye kukumbuka siku zao za kuzaliwa wanaweza fanya hivyo wakiwa kileleni,lakini pia kwa wale wanaoenda Honey Moon baada ya ndoa pia wameshauriwa kufanya hivyo katika kipindi hiki cha ofa.

Baadhi ya watalii wa ndani wakielekea katika kilele cha Shira safari ambayo inatajwa asilimia 70 wanaenda kwa usafiri wa gari.(P.T)

Ukiwa katika hifadhi hiyo utafurahia mandhari mbalimbali za mlima huo.

Wengine wanaweza pia kupanda na watoto wao.


Hivi ndivyo safari ya mwisho huwa.





Njiani utakutana na uoto mbalimbali wa asili .

Zipo tenti kwa ajili ya watalii wanaoendelea na safari.

Waliofanikiwa kufika kilele cha Shira hawakusita kuonesha furaha zao kwa kucheza .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
IDADI ya watalii wanaotembelea hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) imeongezeka kutoka 37,000 hadi kufikia 51,287 ndani ya kipindi cha miaka 10 huku asilimia 4 na sita kati yao wakiwa ni wazawa.
Asilimia hiyo inatajwa ni ya watanzania ambao wamekuwa wakipanda Mlima huo kwa muda wa siku moja hali inayoilazimu uongozi wa hifadhi hiyo kuendelea kuhamsisha wananchi kutembelea hifadhi zetu ili kujionea urithi tuliopewa na Mungu.
Mhifadhi utalii wa KINAPA,Eva Mallya alisema katika kuhamasiosha utalii wa ndani ,KINAPA imeandaa zoezi maalumu ambalo litadumu kwa muda wa siku nne kwa watanzania walio walio karibu na mlima kuweza kuupanda kwa muda wa siku moja na kurudi.
“Tumeandaa zoezi rahisi kwa kila mmoja mwenye nafasi aweze kupanda,sehemu kubwa itakuwa ni kwa kutumia gari ambapo walio tayari watachukuliwa na gari hadi eneo fulani kabla ya kutembea umbali mdogo na kutizama uwanda wa Shira katika mlima Kilimanjaro.”alisema Mallya.
Alisema zoezi la uandikishaji kwa ajili ya watakao penda kupanda katika mlima huo tayari limeanza katika vituo vilivyoko jirani na Duka la Maua mkabala na Rafiki Supermarket ,Hosptali ya rufaa ya KCMC na njia Panda ya Himo.
Mallya alisema mpandaji atapaswa kujitegemea kwa Sweta na Jacket kwa ajili ya baridi ,suruali raba pamoja na chakula huku mhusika akitakiwa kulipia kiasi cha sh 15,000 kama kiingilio cha hifadhini.
Kwa upande wake afisa masoko wa KINAPA,Antypas Mgungusi alisema safari ya kupanda mlima Kilimanjaro imekuwa ikitumiwa na baadi ya watalii kufanya matukio ya kihistoria ikiwemo kufunga ndoa na wengine kuadhimisha siku zao za kuzaliwa wakiwa kileleni.
“Imezoeleka kuwa watu wanapokuwa na matukio yao yakiwemo ya mikutano,au Honey moon baada ya ndoa na siku za kuzaliwa wamekuwa wakifanya sherehe zao mijini,lakini kuna maeneo mengine kama haya ya hifadhi kufanyia mambo hayo”alisema Mgungusi.
Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kwa kuhifadhi barafu kwa kipindi cha mwaka mzima licha ya kupitiwa na mstari wa Ikweta huku ukiwa ndio mlima pekee uliosimama peke yake ukilinganisha na milima mingine duniani.
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI