Wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Iringa wakiwa katika mgomo leo kutokana na
kutopata mkopo kwa wakati ambapo inapelekea kushindwa kabisa kuendesha
maisha yao chuoni hapo baada ya serikali kupitia bodi ya mikopo
kuwacheleweshea pesa zao.
Viongozi
wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakiwatuliza
wenzao leo baada ya mgomo wa wanachuo wa chuo cha RUCU kugoma
wakishinikiza kupewa mikopo yao ili kuendesha maisha chuoni hapo.
Mkuu
wa chuo kikuu ya Iringa Prof Joshua Madumulla akizungumza na wanafunzi
hao baada ya kutokea mgomo chuoni hapo leo asubuhi.
Mmoja
wa wanafunzi wa chuki kikuu cha Iringa akitoa malalamiko yake dhidi
ya bodi ya mikopo kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Angeline Mabula
leo kuhusu kucheleweshewa mikopo yao.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Mabula akizungumza na wanafunzi hao wakati wa mgomo wa wananchuo wa chuo cha RUCU leo
Ulinzi ulikuwa ni wakutosha chuoni hapo (Picha na Francis Godwin)
Jeshi
la polisi mkoani Iringa limelazimika kutumia nguvu kuwatawanya
wanafunzi wa chuo kikuu cha Rucu baada ya kutaka kufanya maandamano na
kusababisha vurugu chuoni hapo.
Kamanda
wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi ameeleza kuwa wanafunzi hao
walitaka kufanya maandamano hayo kwa madai kuwa wamecheleweshewa mikopo
yao.
Kamanda amesema kuwa wamewadhibiti wanachuo hao ili wasitoke nje ya geti la chuo kutokana na kuhofia kuvuruga amani .
Aidha
kamanda ameeleza kuwa jeshi la polisi linawashikilia wanafunzi 89 na
kusema kuwa kwa yoyote atakayejaribu kuvunja amani ni
lazimawatamchukulia hatua kali za kisheria bila kujari chochote.
Hata hivyo wakizungumza wanachuo hao wamesema kuwa kucheleweshwa kwa mikopo hiyo kunachangia maisha yao kuwa magumu.
Wakati
huo huo Jeshi la hilo linawashikilia viongozi watatu wa waendesha
pikipiki kwa tuhuma za kuwafanyia fujo maafisa watatu wa mamlaka ya
usafirishaji wanchi kavu na majini Sumatra.
Kamanda
wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi amesema kuwa maafisa hao
wamefanyiwa fujo wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kawaida katika eneo
la chuo cha mkwawa manispaa ya Iringa.
Kamanda
amesema kuwa jeshi la polisi tayari limeshafungua jalada na watuhumiwa
hao watafikishwa mahakamani muda wowote yatakapoletwa mashtaka.
Aidha
kamanda amesema kuwa endapo matukio kama hayo hayata kemewa mapema
yatachangia uvunjifu wa amani hivyo amewataka wananchi pamoja na
wanahabari kushirikiana kwa pamoja katika kukemea masuala hayo.
Hata
hivyo akizungumza afisa mfawidhi wa mamlaka ya usafirishaji wa nchi
kavu na majini Sumatra mkoa wa iringa Bartel Patel amekiri kufanyiwa kwa
kitendo hicho.
Comments