LIVERPOOL YAIFANYIA CHELSEA KAMA AZAM ILIVYOWAFANYIA YANGA

liver chelsea
Na Richard Bakana-shaffihdauda.com.
Wachezaji wa klabu ya Liverpool jana katika mchezo wa ligi kuu ya England (EPL) walipokutana na mabingwa wapya wa ligi hiyo Chelsea waliwaonyesha heshima yao ya kubeba ubingwa, kitendo ambacho hata hapa Nyumbani Tanzania kwa mara ya kwanza kilionyesha na klabu ya Azam FC ambao waliwapigia makofi Yanga siku ya Jumatano timu hizo zilipokutana katika Uwanja wa Taifa.
YANGABINGWA4
Mchezo huo ambao ulipigwa Nyumbani kwa Chelsea ‘Stamford Bridge’ ulimalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kufungana bao moja moja.
Chelsea ndio walianza kupata bao kupitia kwa nahodha wake John Terry kunako dakika ya tano (5) lakini mkongwe wa Liverpool ambaye anataka kuikimbia timu hiyo Steven Gerrard akasawazisha bao hilo katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na kufanya timu hizo kugawana pointi moja moja na goli 1-1.
chelsea
Gerrard alitumia mchezo huo kuwaaga mashabiki wake ambapo alipotoka Uwanjani dakika za mwisho mwisho za mchezo huo, alienda katika upande wa mashabiki wa Chelsea na kuwapungia mkono na wao wakaonyesha heshima kwa kusimama na kumpigia makofi hari kadharika kwa mashabiki wa Liverpool.
gertard fans
Nguli huyo ambaye maisha yake ya soka yalianzia hapo hapo Liverpool akiwa na miaka nane sasa baada ya msimu huu kumalizika anatarajia kutimkia nchini marekani kumalizia soka lake la uzeeni.
gerard liver

Tuma Maoni


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.