Makabidhiano ya Pampu ya Maji Kisima cha Kaburi Kikombe na Utilianaji Saini wa Mradi wa Uchimbaji Kisima Bomani

      

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu akitiliana
saini ya makubaliano ya Mrai wa Uchimbaji wa Kisima katika maeneo ya Bamani na
Mwenyekiti wa Tanzania Youth Icon, Ndg Abdullah Miraji Othman, mradi huo
utaharimu shilingi za kitanzania milioni mia tatu, utilianaji wa saini hiyo
umefanyika katika Ofisi za ZAWA Mabuluu

 WANANCHI wa Jimbo la Kikwajuni wakishuhudia utilianaji wa
saini ya makubaliano ya Mradi wa Uchimbaji wa wa kisima cha Maji Safi na Salama
kwa Wananchi wa jimbo hilo.
MKURUGENZI
wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu akibadilishani
Mikatabani ya makubaliano ya Mradi wa Uchimbaji wa Kisima katika maeneo ya
Bomanii Unguja Mradi huo utagharimu shilingi milioni Mia tatu, akibadilisha na
Mwenyekiti wa Tanzania Youth Icon, Ndg Abdullah Miraji Othman, mradi huo
utaharimu shilingi za kitanzania milioni mia tatu, utilianaji wa saini hiyo
umefanyika katika Ofisi za ZAWA Mabuluu.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe. Eng.Hamad Yussuf
Masauni akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kutiliana saini ya Makubaliano ya Mradi
wa Uchimbaji wa Kisima, mradi unaosimamiwa na Tanzania Youth Icon.
Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa Afisi za ZAWA
Mabluu Unguja wakifuatilia makubaliano hayo.
Mheshimiwa
Meya ya Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khati na Diwanj wa Kikwajuni Mhe
Mahboob wakishuhudia utilianaji wa saini hiyo ya makubaliano ya Mradi wa Maji
Awamu ya Pili kwa Jimbo hilo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa
Ali Garu akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini ya Makubaliano
ya pande hizo mbili yaliofanyika katika Afisi Kuu ya ZAWA  Mabluu Zanzibar.
Waheshimiwa
wakifuatilia hafla hiyo ya utilianaji wa Saini ya Mradi wa Uchimbaji wa kisima
cha Maji Safi na Salama kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, mradi huo
unaosimamiwa na Tanzania Yuoth Icon na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA)
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng. Hamad Yussuf Masauni,
akimkabidhi mashine ya Pump ya Maji ya Mradi wa Kwanza wa Kisima cha Kaburi
Kikombe, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dk Mustafa Ali Garu,  ambao uko katika hatua za mwisho ya ufungaji
wa Pump hiyo na tayari kwa kutowa huduma ya maji kwa wananchi wa Jimbo lake.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng. Hamad Yussuf Masauni,
akimkabidhi  Pump ya kuvutia maji kwa
ajili ya kisima kipya cha Kaburi Kikombe, Mkurugenzi  Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa
Ali Garu.kwa ajili ya Mradi wa Kwanza wa Uchimbaji wa Kisima cha Kaburi Kikombe
ambao uko katika hatua za mwisho ya ufungaji wa Pump hiyo na tayari kwa kutowa
huduma ya maji kwa wananchi wa Jimbo lake.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu, akitowa shukrani kwa Mlezi wa Jumuiya ya Tanzania Youth Icon (TAYI) kwa ushirikiano wa Taasisi hiyo na ZAWA, katika jitihada zake za kukamilisha Mradi Mkubwa wa Kisima huko Kaburi Kikobe na kutiliana saini ya makubaliano ya Mradi wa Pili wa Uchimbaji wa Kisima katika eneo la bomani Unguja ukiwa na thamani ya shilingi milioni mia tatu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.