MVUA ZA MASIKA KUKOMA MEI MWISHONI

Mkurugenzi Mtendaji wa TMA, Agnes Kijazi
                                  Mkurugenzi Mtendaji wa TMA, Agnes Kijazi
MVUA za masika zinazoendelea kunyesha zinatarajiwa kukatika mwishoni mwa mwezi huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alisema hayo alipokuwa akizungumzia mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.
Alisema ndani ya msimu huu wa mvua kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua nyingi.
"Mfano mvua zilizonyesha Zanzibar zimenyesha kwa muda mfupi, lakini kwa wingi hadi kuleta mafuriko."Zanzibar mafuriko yaliyotokea juzi saa tatu asubuhi kituo cha mamlaka kilipima milimita 196.1. Mei tatu mwaka huu ilinyesha masaa machache kituo kilipima milimita 172.2. Hii ndiyo ilileta mafuriko," alisema Dk Kijazi.
Alitoa angalizo wananchi wajitahidi kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamlaka hiyo ili kuepuka kupata matatizo.CHANZO: HABARI LEO (Muro)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA