NOOIJ AWAANZISHA NDEMLA, OSCAR JOSHUA TAIFA STARS NA SWAZILAND LEO

Na Mahmoud Zubeiry, RUSTENBURG
KOCHA Mart Nooij amemuanzisha kiungo chipukizi, Said Hamisi Ndemla pamoja na John Bocco kama mshambuliaji pekee katika mchezo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya Swaziland usiku wa leo Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace mjini hapa.
Maana yake, Mholanzi huyo, atatumia viungo watatu usiku wa leo, pamoja na Ndemla, wengine ni Erasto Edward Nyoni na Mwinyi Kazimoto Mwitula.
Mchezo huo wa Kundi B Kombe la COSAFA utaanza Saa 1:30 usiku, saa moja zaidi kwa saa za nyumbani, Tanzania na utatanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Lesotho na Madagascar itakayoanza Saa 11:00 jioni.
Mrisho Ngassa na Simon Msuva watacheza kama washambuliaji wa pembeni (mawinga).
Said Ndemla (kushoto) ataanza leo Taifa Stars ikimenyana na Swaziland leo mechi ya kwanza Kombe la COSAFA

Safu ya ulinzi, langoni ataanza Deo Munishi ‘Dida’, kulia Shomary Kapombe, kushoto Oscar Joshua na katikati Salim Mbonde na Aggrey Morris.
Katika benchi watakuwapo; Mwadini Ali, Abdi Banda, Mwinyi Hajji Mngwali, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Hassan Dilunga, Ibrahim Hajib na Juma Luizio, wakati Said Makapu atakuwa jukwaani kabisa kwa sababu ni majeruhi.
Kuelekea mchezo huo, Mholanzi Nooij anataka kuendeleza mafanikio yake katika michuano ya COSAFA wakati anafundisha Msumbiji kabla ya kuja Tanzania.
“Hii si mara ya kwanza kwangu kama kocha kushiriki mashindano haya ya COSAFA,” alisema jana. “Nchi wanachama wa COSAFA zote zina timu madhubuti za taifa, ambayo inafanya michuanno iwe ya ushindani. Hicho ndiyo ambacho tunakitafuta timu ya taifa ya Tanzania,”.
Kikosi kinachoanza; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Said Ndemla na Simon Msuva.
Benchi; Mwadini Ali, Abdi Banda, Mwinyi Hajji Mngwali, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Hassan Dilunga, Ibrahim Hajib na Juma Luizio.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI