OFISI YA RAIS,TUME YA MIPANGO:TUME YA MIPANGO YATEMBELEA EPZA


 Mandhari ya kuvutia ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) yaliyopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa mabinti wa Kitanzania walioajiriwa na Tooku Garments akiwa kazini.
 Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiangalia moja ya suruali zinazotengezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.
 Bibi Lilian Kalengo (Kulia), muwakilishi wa Kiwanda cha Tooku Garments akiwaonesha suruali ya jeans wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam. Kiwanda hicho ni moja ya viwanda 12 vilivyoanza uzalishaji katika Ukanda wa huo.
 Wakina dada wakiendelea na kazi ya utengenezaji wa suruali za jeans zinazotengenezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).

 Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) akizungumza na Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) wakati Bibi Mwanri na ugeni wake walipotembelea Ofisi za Mamlaka kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).
Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mhandisi Keneth Haule (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Abel Shirima (Kushoto), Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), na Bw. Omary Abdallah (Wapili Kulia).PICHA NA SAIDI MKABAKULI

0 comments:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA