RAIS WA BURUNDI NKURUNZINZA APINDULIWA

Rais wa Burundi
 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza kufungwa kwa mipaka
1 Mwandishi wa BBC huko Bujumbura Kazungu Lozy anasema watu wangali wanasheherekea Rais Nkurunzinza ameingia ndani ya gari lake na kuondoka mjini Dar es Salaam akionesha dalili kuwa yuaelekea BurundiKiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare
18:37 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ameamrisha wanajeshi kuzuia rais Nkurunzinza kutua Burundi
18:30 Rais Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuhutubia taifa baada ya kurejea kutoka Tanzania amesema msemaji wake Willy Nyamitwe.Wananchi waendelea kusheherekea Bujumbura kufuatia tangazo la ''Mapinduzi''
18:25 Generali Niyombareh ametoa amri kwa majeshi kuungana na kulinda viwanja vya ndege kote nchini humo
18:20 Generali aliyeongoza ''Mapinduzi'' leo asubuhi amewataka maafisa wa jeshi na polisi kufanya kazi kwa pamoja ilikulinda usalama wa nchi hiyo.Rais kikwete alipohutubia waandishi wa habari Dar es Salaam akiandamana na Rais Nkurunzinza

18:15 Viongozi wa kanda ya Afrika wametaka makundi hasimu kutulia na kukubali hali ya kikatiba Kurejea

18:10 Esipisu amesema kuwa rais Uhuru Kenyatta anaunga mkono kurejeshwa kwa utawala wa kikatibaMaafisa wa jeshi la Burundi wakisheherekea Barabarani Bujumbura

18:07 Msemaji wa rais wa Kenya Manoah Esipisu amesema kuwa viongozi wanataka hali ya kawaida irejee huko BurundiRais Uhuru Kenyatta akiwa Tanzania

18:06 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi

18:05 Rais amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki

18:01 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.Raia wakisheherekea ''Mapinduzi''

18:01 Viongozi hao wanakutana dar es salaam kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi

18:01 Rais Jakaya Kikwete amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki

18:00 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi

17:55 Msemaji wa rais Nkurunzinza ameiambia BBC kuwa asilimia 95 ya taifa hilo ingali salama na wala hakuna tashwishi.Manuari za kijeshi zingali barabarani mjini Bujumbura

17:50 Manuari zaidi zaonekana barabarani mjini Bujumbura

17:45 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.

17:30 Msemaji wa rais Nkurunziza,Willy Nyamitwe ameiambia BBC kuwa rais huyo angali madarakani na kuwa hajaondolewa madarakaniRaia wakiwazoma maafisa wapolisi ambao awali walikuwa wakikabiliana nao

17:22 Redio ya taifa ya Burundi inasema kuwa rais Nkurunzinza angali Madarakani na kuwa hakujakuwa na ''mapinduzi''Raia wakikumbatiana katika bustani la uhuru Bujumbura

17:20 Maafisa wa jeshi wanaolinda kituo cha taifa cha redio wamewaonya watangazaji wasitangaze kuwa kuna ''mapinduzi''

17:05 Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema kuwa waandamanaji wamefululiza hadi kwenye vituo vya polisi na magereza yaliyokuwa na mahabusu waliokamata kwa kuandamana na kuwaachilia huruWanajeshi ya Burundi wakijaribu kutuliza hali Bujumbura

17:00 Redio ya taifa inasema kuwa bado rais Nkurunzinza angali madarakani.

16:50 Kituo hicho cha redio cha ''African Public Radio'' kinapeperusha tangazo la kupinduliwa kwa serikali ya rais NkurunzinzaRaia wanasherehekea ''kupinduliwa'' kwa Nkurunzinza

16:40 Redio iliyokuwa imefungwa na serikali ya rais Nkurunzinza kwa kupeperusha habari za maandamano imefunguliwa upya.

16:30 Mwandishi wa BBC Cyriac Muhawenay aliyeko Bujumbura anasema raia wanaonekana kuwa na furaha.

16:20 Picha za raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshiVifaru vya kijeshi katikati ya mji mkuu Bujumbura

16:08 Watu wanaonekana wakininginia kwenye vifaru vya jeshi

16:05 Afisi ya urais nchini Burundi imetangaza kwenye mtandao wake wa twitter kuwa ''hali ni Shwari''Raia wakishangilia ''mapinduzi''

16:00 Majeshi wameonekana nje ya kambi za kijeshi mjini Bujumbura

15:58 Viongozi wa jeshi wamewaamrisha maafisa wa polisi kuondoka mabarabarani.Raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi Bujumbura

15:55 Mwandishi Sonia Rolley, wa Radio France International anasema kuwa halaiki ya raia wamefika nje ya kituo hicho wakishangilia matukio hayoWaandamanaji Bujumbura

15:50 Waandamanaji wanasemekana kuambatana na wanajeshi kuelekea katikati ya mji mkuu wa Bujumbura

15:45 Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake.Waandamanaji Bujumbura

15:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Maud Julien anasema kuwa Miili ya watu watatu imeonekane katika barabara za Bujumbura

15:36 Viongozi wote wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wako Dar es Salaam kwa mwaliko wa rais Kikwete.Raia wanashangilia mjini Bujumbura
15:35 Rais Nkurunzinza yuko mjini Dar es Salaam Tanzania kuhudhuria mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisasa uliokuwa ukiendelea Burundi.
15:30 Maelfu ya raia wa Burundi waandamana a mabarabarani mjini Bujumbura wakishangilia tangazo hilo la ''kutomtambua'' rais Nkurunzinza.Maafisa wa jeshi la Burundi wanaonekana wakiweka usalama
15:20 Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
15:10 Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuwania awamu ya tatu
15:05 Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
15:00 taarifa zaibuka kutoka Burundi kuwa rais Nkurunzinza ameng'olewa'' madarakani.
Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa BurundiPolisi wameamrishwa kuondoka mabarabarani
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.Raia wa Bujumbura wakishanilia tangazo la generali Niyombareh
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi

Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.

Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi
Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''
CHANZO BBC SWAHILI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI