TUSKER YAJA NA FANYAKWELI KIWANJANI


Tusker Lager kupitia kampeni yake ya “Fanya kweli” wiki hii inawaletea wateja wake shindano la wiki lilopewa jina la “Fanya kweli Kiwanjani”. Shindano hilo litahusisha baa mbalimbali za mitaani tunapoishi ndani ya jiji la Dar Es Salaam. Kampeni hii ya “Fanya Kweli” imekua na lengo la kuhamasisha watanzania kujitengenezea maisha mazuri ya baadaye kupitia juhudi zao binafsi pamoja na msaada wa wadau ambapo kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuhamasisha na kubadilisha fikra za watanzania wengi kupitia vipindi na matamasha yanayolenga kuthamini watanzania wenzetu waliofanikiwa katika maisha na hivyo kuwapa motisha watu wengine kufuata nyayo zao. Shindano hili ambalo litadumu kwa takriban muda wa wiki tano, linatazamia kutoa zawadi mbalimbali kwa wapenzi wa bia ya Tusker na baa zao wanazozipenda ambapo zaidi ya baa 50 jijini Dar es salaam zinatarajiwa kushiriki kikamilifu kwenye shindano hilo. Kati ya baa 50 zitagawanywa kwenye makundi ya baa 10 kwa wiki ambapo zitapewa promo nzito wiki husika kupitia kituo cha redio cha E-fm kwenye kipindi cha “Ubaoni” kinachorushwa kati ya saa tisa mchana mpaka saa moja usiku na watangazaji wake mashuhuri, Gardner G. Habash na Seth wataipa promo kampeni hii nzima pamoja na kuwakumbusha wapenzi wa baa zinazoshindana kushiriki kwenye kampeni hii. Watangazaji hawa pia watagawana baa 5 kati ya 10 zitakazo shindanishwa, kisha kuwaomba wasikilizaji wao kuchagua baa 1 bora na baa itakayoibuka mshindi kituo cha radio cha E-fm kitafunga kambi ndani ya baa hiyo na kuwafanyia sherehe pamoja na kukabidhi zawadi mbalimbali. Watangazaji hawa pia watatoa maelekezo ya jinsi gani wasikilizaji watakavyoweza kuzipigia kura baa wazipendazo na pia jinsi ya kushinda zawadi ndogo ndogo zitakazotolewa kwa wasikilizaji wa kipindi hicho cha redio. Kupitia shindano hili, Tusker imedhamiria kusaidia katika kuzitangaza zaidi baa maarufu za mitaani tunapoishi sambamba na kuibua sifa za huduma nzuri zitolewazo na baa hizo huku pia ikionekana kama njia ya kuwaongezea mauzo kwa ujumla. Kuna njia mbalimbali ambazo mashabiki wa Fanya kweli kiwanjani wanaweza kuzitumia katika kuzipigia kura baa wazipendazo ambapo anachotakiwa mtu kufanya ni kutembelea baa ya mtaani kwake na kunywa bia ya Tusker, kupiga picha na kisha kuweka picha hizo kwenye kurasa za jamii (Facebook na Twitter) za Tusker au kusikiliza E-fm kwa maelekezo zaidi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.