UJUE WASIFU MWANANA WA PROFESA MUHONGO

Uongozi wenye Dira, Ubunifu na Ugunduzi – Uaminifu, Uadilifu na Kujituma – Stadi Bulibuli za Usimamizi na Uzoefu katika Uongozi – Uwazi na Ufanisi – Matokeo Yenye Tija na Ubora wa Hali ya Juu

New PictureProf Dkt Sospeter Muhongo, mwanazuoni maarufu, mwanajiolojia mbobevu na Mbunge wa Kuteuliwa, amewahi kuwa Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (April 2012- Januari 2015). Serikali ya Ufaransa ilimtunukia Cheo cha Afisa Mwenyetunu ya Kitaaluma Iliyotukuka – Ordre des Palmes AcadΓ©miques (Iliyoanzishwa na Mfalme NapolΓ©on Mwaka 1808) na ni mtu wa kwanza kupokea Tuzo (Mwaka 2004) inayoheshimika sana kwa Jamii ya Wanajiolojia wa Afrika ya Prof Robert Shackleton (UK) (Geological Society of Africa’s prestigious Prof Robert Shackleton Award), kwa ajili ya utafiti wa kipekee kuhusu Jiolojia ya Afrika ya miamba yenye umri wa zaidi ya miaka Milioni 500 (Precambrian Geology of Africa). Kwa kutambua mchango wake mkubwa wa kimataifa katika Sayansi na Ustawi wa Jamii ulimwenguni, Prof Muhongo amepewa nafasi nyingi zenye kuheshimiwa na wasomi na wataalamu maarufu Duniani, pamoja na kutambulika kwa ngazi za juu kabisa na Vyama na Taasisi zao za kitaaluma, kwa mfano: An Honorary Fellow of the Geological Society of London (Ilianzishwa Mwaka 1807), Honorary Fellow of the Geological Society of America (Ilianzishwa Mwaka 1888), an Honorary Research Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (Ilianzishwa Mwaka 1956). Ni Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Akademia ya Sayansi ya Nchi Zinazoendelea (FTWAS), Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Chama cha Wanajiolojia wa Afrika (FGSAf) , Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Akademia ya Sayansi ya Afrika (FAAS) na Mshiriki wa Ngazi ya Juu (Fellow) wa Akademia ya Sayansi ya Tanzania (FTAAS) na nyingine kadhaa. Ni Makamu wa Rais Mstaafu wa Tume ya Ramani ya Jiolojia ya Dunia (CGMW) na pia Mhariri Mkuu Mstaafu wa Jarida la Afrika la Sayansi za Miamba na Madini (The Journal of African Earth Sciences, Elsevier). Prof Muhongo ni Mshindi wa Mwaka 2014 wa Tuzo ya Heshima ya Jamii ya Wanasayansi wa Jiolojia na Uchimbaji Petroli na Gesi Asilia ya Nigeria (NMGS)/AMNI ya Prof M.O. Oyawaye. Prof Muhongo aliongoza na kusimamia mabadiliko endelevu ya ubunifu na ugunduzi katika Sekta za Nishati na Madini nchini mwetu kwa kuingiza sera mpya na kutengeneza nyaraka za kisheria, ameongeza idadi kwa wingi ya rasilimali watu iliyopata mafunzo mazuri ya kitaaluma katika Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia. Amesimamia ongezeko la kasi kubwa ya kampeni ya usambazaji umeme vijijini, na amesimamia usambazaji wa haraka na wa uhakika wa umeme mijini. Amesimamia punguzo kubwa la gharama za kuunganishiwa umeme vijijini na mijini. Amesimamia ongezeko la mapato katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kutokana na kodi na tozo mbalimbali kwenye madini yetu. Baadhi ya wachimbaji wadogo wamepatiwa mafunzo na ruzuku ya kuboresha uchimbaji wao. Tarehe 28.02.2015, Chama cha Wachimbaji Wadogo nchini (FEMATA) kilimteua, kwa kauli moja, Prof Muhongo kuwa Mshauri Mkuu wao. Prof Muhongo alisimamia utayarishaji wa mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Umeme nchini, ikiwemo TANESCO, na Juni 2014 Wizara ya Nishati na Madini ilitangaza mipango na miradi itakayotekelezwa kuhakikisha Taifa linapata umeme mwingi wa kutosha mahitaji yake, umeme unaopatikana kwa urahisi na kwa uhakika, umeme wa bei nafuu na umeme wa ziada (biashara) kwa manufaa ya uchumi wetu – Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap 2014-2025, Powering Vision 2025. 2 Prof Muhongo amevutia uwekezaji mpya (kutoka ndani na nje ya nchi) wenye mitaji midogo na mikubwa kwenye Sekta za Nishati, Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Haya yote yamechangia ukuaji mzuri wa uchumi wetu. Yeye ni Profesa Kamili (mstaafu) wa Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Profesa wa Heshima wa Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini. Ni mjumbe wa bodi kadhaa za uhariri wa majarida ya sayansi na vijarida vya sayansi, teknolojia na ubunifu. Yeye ni Mhariri Mwandamizi wa Kitabu cha Mwaka 2009 kiitwacho: Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii: Simulizi za Mafanikio kutoka Afrika (“Science, Technology and Innovation for Socio-Economic Development: Success Stories from Africa”). Prof Muhongo na watafiti wenzake wamechapisha ramani kwa kuzingatia dhana na maarifa ya kisasa ya Jiolojia, kama vile: Jiolojia na Mashapo Makubwa ya Madini ya Afrika, Jiolojia na Mashapo ya Vito vya Thamani vya Afrika Mashariki na Ramani ya Jiolojia na Madini ya Tanzania. Hakuna mikopo au misaada ya fedha ilitumika kutengeneza ramani hizi. Ramani hizi zinatumika kupanua na kukuza uwekezaji mpya katika Sekta ya Madini Barani Afrika. Prof Muhongo alikuwa Rais wa Chama cha Wanajiolojia wa Afrika (1995-2001). Alikuwa Mkurugenzi Mwanzilishi (2005-2010) wa ICSU Ofisi ya Sayansi ya Kanda ya Afrika, Pretoria, Afrika Kusini. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya UNESCO-IUGS-IGCP Programu ya Kimataifa ya Sayansi ya Jiolojia (2004- 2008), na Mwenyekiti (2007-2010) wa Kamati ya Programu ya Kisayansi (SPC) ya Mwaka wa Kimataifa wa Sayari ya Dunia uliotangazwa na Umoja wa Mataifa (UN-IYPE). Prof Muhongo aliteuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mgombea (2009) wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO. Alikuwa Mwenyekiti (1999-2005) wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO), Tanzania; na alikuwa Mkuu wa Idara ya Jiolojia, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (1997-2000). Prof Muhongo alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi ya Serikali ya Tanzania kuhusu ajali mbaya ya vifo katika migodi ya Mererani (2002). Prof Muhongo alisimamia kwa umakini mkubwa uboreshaji wa rasilimali watu, majukumu, miradi na utendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC). Prof Muhongo amechapisha zaidi ya makala (publications) 200 za sayansi ya hadhi ya juu zikiwa ni za kiutafiti zenye kukubaliwa na kurejelewa na watalaamu Duniani kote. Ametoa mihadhara ya kisayansi zaidi ya 500 akiwa ndiye Mzungumzaji Mkuu (Keynote Speaker) katika Mikutano ya Kimataifa na Kitaifa. Kwa zaidi ya miongo miwili, Prof. Muhongo ameandaa vikao zaidi ya 100 vya mikutano ya vikundi vya wataalamu wa Kitaifa na Kimataifa vya sera, teknolojia na sayansi za nishati, miamba, madini, maji, tabianchi na mazingira. Amekuwa Mwandishi Mkuu wa mikutano ya sera za sayansi ikiwa ni pamoja na “Sayansi na Afrika” ambayo inadhaminiwa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (UNECA), Kamisheni ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) na washirika wake. Prof. Muhongo amepata tuzo mbalimbali za kiuanazuoni na kitaalamu, ametambuliwa na kupata hibafedha kwa kazi mbalimbali za kitaaluma pamoja na kutunukiwa fedha za utafiti. Ameshirikiana na wanasayansi mabingwa wa Mabara yote kwenye tafiti za kisayansi. Alisomea Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania) na GΣ§ttingen (Ujerumani). Alihitimu na kutunukiwa shahada ya Dr.rer.nat. kutoka Technical University of Berlin, Ujerumani. Prof. Muhongo anaongea, na kuandika kwa ufasaha na umahiri mkubwa Kiswahili, Kiingereza na Kijerumani, na kwa wastani kwa lugha ya Kifaransa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU