UVCCM MKOA WA IRINGA WAMPA TUZO YA UONGOZI BORA KATIBU MKUU UVCCM SIXTUS MAPUNDA



katibu  wa  UVCCM mkoa  wa  Iringa Elisha Mwampashi wa  pili  kulia akimkabidhi tuzo maalum ya uongozi bora  katibu  mkuu  wa UVCCM Taifa Bw  Sixtus Mapunda  kushoto leo  wakati wa kikoa  cha tathimini ya  ziara  yake  mkoani Iringa
Katibu  mkuu wa UVCCM Taifa Bw Sixtus Mapunda  akionyesha  tuzo  maalum ya  uongozi  bora  aliyokabidhiwa na  UVCCM mkoa wa Iringa kushoto ni mjumbe wa baraza kuu la  utekelezaji  vijana Taifa Bi Secky  Kasuga  na kulia ni katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Elisha Mwampasha
Vingozi wa vijana mkoa wa  Iringa wakiwa katika kikao  cha tathimini ya  ziara ya katibu mkuu  wao Taifa
Na Matukiodaima Blog

UMOJA wa  vijana  wa chama  cha mapinduzi (UVCCM)  mkoa  wa Iringa umempatia tuzo  maalum ya uongozi  bora  katibu mkuu  wa  UVCCM Taifa  Bw  Sixtus Mapunda baada ya  kazi  kubwa ya  kukijenga  chama  aliyoifanya ndani ya  wilaya za  mkoa  wa Iringa .

Katibu  wa  UVCCM mkoa wa Iringa  Bw  ElishaMwampasha  amekabidhi   tuzo  hiyo  leo  wakati wa kikao  cha tathimini ya  ziara  yake ya  siku  tatu  mkoani  Iringa .

Alisema kuwa UVCCM Taifa  imepata  kuwa na makatibu wengi ila  utendaji kazi na uwajibikaji  wa  vitendo  ambao  ameufanya katibu  huyo Bw Mapunda ndani ya mkoa wa Iringa ni wa mfano na wao kama  vijana  wamependezwa na utendaji wake  hivyo  kulazimika  kutoa tuzo hiyo kama ishara ya  kumpongeza na kumtia  moyo  ili  kuzidi  kuendelea na utendaji huo .

"Mheshimiwa katibu mkuu wa UVCCM Taifa sisi  vijana  wa mkoa wa Iringa  tumependezwa na utendaji kazi  wako na  wewe  ni mmoja kati ya viongozi wa  mfano katika Taifa letu hivyo  tunaomba  kukutunuku tuzo ya maalum ya  heshima  ya  uongozi  bora "

Katika hatua  nyingine  katibu  huyo wa UVCCM mkoa wa Iringa alimpongeza Bw Mapunda kwa  kuchangia  shughuli mbali mbali za maendeleo katika ziara  yake na  kuwa agizo lake la kuwataka  vijana kusaidia  ujenzi wa  bweni la  wanafunzi shule ya  sekondari Idodi ambalo  liliungua moto wamelipokea na  watafanya  zaidi ya  kufyatua  tofari  wataanza  ujenzi hata kwa  kuchimba  msingi .

Kwa  upande  wake Bw Mapunda  mbali ya  kuwashukuru  vijana hao  kwa  kutambua mchango  wake  ila  alisema kazi hiyo anayoifanya  ni sehemu ya majukumu yake na hakutegemea  kupewa  tuzo  hiyo ya heshima kwani kama ni  sifa  ni za  vijana  wote nchini ambao  wanatoa ushirikiano kwake .

"Sikutegemea kama  mmeniandalia  tuzo hii  mimi  kuja  huku  Iringa na kufanya  yote  niliyoyafanya ni kwa ajili ya  kujenga  chama  chetu  sote na  kuwaonyesha  wapinzani kuwa CCM ni kazi kwa  vitendo zaidi na sio porojo  za majukwaani ambazo hazina faida kwa  wananchi"

Ziara  ya  kiongozi  huyo mkoani Iringa  imeonekana  kuwa na matumaini mapya kwa  CCM katika  jimbo la Iringa mjini  ambalo  linaongozwa na mbunge  mchungaji Peter Msigwa (Chadema)  ambae amesema kuwa  muda  wake wa  kukabidhi jimbo  CCM umefika na kuwataka CCM hasa  vijana  kutofanya  siasa za wapinzani za maneno na badala  yake  kushiriki katika  shughuli za maendeleo na  wananchi.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.