VIKONGWE WANASWA NA MAGOBOLE



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari
JESHI la Polisi mkoani Katavi linawashikilia watu tisa wakiwemo vikongwe wa miaka 80 na 70 baada ya kukamatwa wakiwa na bunduki tatu za kienyeji aina magobole, risasi zake 15, mtambo wa kutengenezea silaha, baruti na sare za Jeshi la Wananchi la Ulinzi na Usalama (JWTZ).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari alitaja vitu vingine vilivyokamatwa kufuatia msako mkali unaoendelea wilayani Mlele ni vipande tisa vya nondo, vyuma vya kutengenezea risasi na mafuta ya kiboko yaliyohifadhiwa kwenye chupa.
"Mafanikio haya yametokana na ushirikiano mzuri kati Jeshi la Polisi, askari wa Tanapa na raia wema ambapo wamekuwa wakiendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kufanikisha katika ukamataji," alieleza .
Alidai kuwa silaha hizo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na zilikuwa zikitumika katika visa vya kijangili na uhalifu mwingine wilayani Mlele.
Akizungumza kwa njia ya simu, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Lazaro Zakaria (63) aliyekamatwa akimiliki gobole bila kuwa na kibali, Shaaban Mussa (52) gobole bila kuwa na kibali na Robert Kaumba (80).
Wengine ni Hamisi Rehani (70) alikamatwa akiwa na mtambo wa kutengenezea silaha aina ya gobole bila kuwa na kibali, Benedict Simon (52) akiwa na risasi 15 za gobole, vipande tisa vya nondo, vipande vya miti, mtutu mmoja na baruti ndani ya chupa na Shaaban Mussa (52) alikamatwa akiwa na risasi moja ya gobole bila kibali.
Kwa mujibu wa Kidavashari, katika msako huo pia jeshi hilo lilimtia mbaroni Esther John (21) akiwa na sare ya JWTZ na vyuma viwili vya kutengenezea risasi na Mashaka George (32), alikamatwa akiwa na mafuta ya kiboko aliyoyahifadhi kwenye chupa.
Alieleza kuwa watuhumiwa wote, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa upelelezi na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.CHANZO: HABARI LEO (Muro)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.