Wabongo wajitokeza kuilaki Taifa Stars ikitua Rustenburg

Baadhi ya Wachezaji wa Taifa Stars baada ya kuwasili Afrika kusini
TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili leo mchana majira ya saa 6 kamili katika jiji la Rustenburg na kufikia katika hoteli ya Hunters Rest – Protea iliyoypo pembeni kidogo ya jiji.
Taifa Stars ambayo iliondoka jana joni jijini Dar es salaam jijini Dar es salaam na kufika OR Tambo saa 5 usiku, ilipata mapokezi mazuri kutoka kwa waandaji wa michuano ya COSAFA pamoja na watanzania wanaoishi jijini humo, ililala katika hoteli ya Southern Sun.
Safari ya kutoka Johannesburg kuelekea Rustenburg ilichukua takribani masaa mawili na msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ephaphra Swai.
Baadhi ya Watanzania waishio Afrika kusini walijitokeza uwanja wa Ndege kuipokea Taifa Stars
Wachezaji waliopo na timu Rutsenburg ni Deogratius Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Salim Mbonde, Aggrey Moriss, Joram Mgeveke, Said Juma, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto, Ibhrami Ajib, Juma Luizio, John Bocco, Mrisho Ngasa na Saimon Msuva.
Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kufanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Rustenburg Impala Bowling Club majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Kusini sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.
Watanzania walijitokeza kuipokea Taifa Stars

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU