WATEJA WA TIGO NCHINI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA TAASISI YA “EduMe” KATIKA ELIMU

 

               

indexKampuni yenye ubunifu zaidi wa kidijitali nchini na EduMe, inayotoa huduma ya kwanza ya kimataifa ya mambo ya elimu kupitia simu wamezindua bidhaa ya kipekee ya ujasiriamali kwenye simu kwa wateja wa Tigo nchini Tanzania.
Shule ya Biashara inawawezesha watumiaji kujifunza ujuzi wa biashara na ujasiriamali kwa bei nafuu kabisa kupitia kwenye simu yoyote ya mkononi. Tigo Tanzania, ambayo ni sehemu ya kampuni ya kimataifa ya mawasiliano ya simu na vyombo vya habari ya Millicom, ni ya kwanza barani Afrika kuzindua huduma kama hii.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha kidijitali Bw. Yaya N ‘Djore alisema” Kampuni ya Tigo Tanzania ilituzwa ruzuku YA ubunifu kutoka GSMA Connected Women ili kutengeneza huduma ya “Shule ya Biashara” mafunzo ya ujasiriamali wa kwenye simu yanayolenga kuwaandaa wajasiriamali wenye kipato kidogo kuwa na ujuzi unaohitajika kuanza au kukuza biashara “
Somo linatumia hadithi za wamiliki wa biashara wa ndani na masomo yaliyochambuliwa ili kutoa mwongozo kwa watumiaji kupitia kila hatua muhimu ya kuanzisha na kuendesha biashara. Masomo yanaelezea mada kama vile, jinsi ya kuchagua wazo la kibiashara, jinsi ya kuongeza uelewa kuhusu biashara na jinsi ya kusimamia biashara yako. Masomo yanatolewa kwa njia ya ujumbe mfupi au sauti kwa lugha ya Kiswahili na kufanya yapatikane kwenye simu yoyote, na kwa watu wenye uelewa mdogo wa lugha ya kiingereza na / au ngazi ya elimu. Baada ya kukamilisha masomo watumiaji wanaweza kupata vyeti vya ujasiriamali vya EduMe-Tigo. Pia watapata fursa ya kuomba mikopo midogo kupitia kwenye ushirikiano wa Tigo na Benki ya Afrika na Benki ya Wanawake ya Covenant (Tanzania) Ltd.
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania Bw. Diego Gutierrez, alisema: “Tumefurahi kutoa huduma hii kubwa na mpya kwa wateja wetu. Kuna mahitaji makubwa ya elimu ya biashara nchini Tanzania kwa sababu wajasiriamali ndio wanaounda uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Kampuni ya Tigo ina dhamira ya kukuza maisha ya kidijitali na kubadilisha maisha. Elimu ni muhimu katika hili.”
Mkurugenzi Mtendaji wa EduMe Bw.Jacob Waern, alielezea: “Tumefurahi kutoa fursa kwa mamilioni ya watu nchini Tanzania kupata mafanikio katika biashara zao. Dhamira yetu ni kuanzisha huduma mpya za simu zinazohusu elimu ambazo zitawawezesha wateja wetu kujifunza kwa wakati wowote na mahali popote.
Kutokana na kujikita kwao kwenye ubunifu katika masoko ya ndani na dhamira yao ya kutoa huduma tofauti kwa wateja, Kampuni ya Tigo ni mwenza sahihi wa EduMe.”
Huduma ya Shule ya Biashara inapatikana kwa wateja wa Tigo. Wateja wanaweza kupata huduma hii kwa kupiga * 148 * 33 # au kwa kutuma ujumbe wenye neno Biashara kwenda 15633.
Ingawa huduma ilifunguliwa kwa watumiaji wachache mwezi Oktoba 2014, huduma mpya ambayo ni rahisi kwa watumiaji sasa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo. Hadi sasa, Shule ya Biashara ya Tigo imetoa zaidi ya masomo 100,000. Zaidi ya watumiaji 11,000 wameshatumia huduma hii, kati ya hao watumiaji 4,000 ni wanawake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI