Airtel yazindua ofa ya LUKU DAR ES SALAAM

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari leo katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam Juni 23, 2015 wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kupata Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money (Kulia) Meneja wa Airtel Money.Steven Kimea.
Meneja wa Airtel Money Steven Kimea (Kulia) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kujipatia nyongeza ya Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, anayefwata kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.

Picha na Philemon Solomon-Fullshangweblog
……………………………………………………
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika la umeme la (TANESCO) imezindua ofa kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima Unit za bure za Luku pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money.
Ofa hii mpya ina lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme na pia kuwazawadia wateja wa Airtel wanaonunua unit za LUKU kupitia huduma ya Airtel Money.
Akiongea kuhusu ofa hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackosn Mmbandoalisema” Wateja wetu watazawadia unit LUKU za ziada Bure mara tu watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money. Tunaamini ofa hii inaendana na mahitaji na mwendendo wa maisha ya watanzania. Kwa sasa manunuzi ya umeme kupitia njia nyingine si tu yanaleta changamoto za kusafiri umbali mrefu na kupoteza muda mwingi kupata huduma bali husababisha watu kukaa foleni ndefu kusubiri kununua umeme. leo Airtel tunatoa ofa hii kwa wateja wetu na kuwawezesha kununua LUKU kwa urahisi wakiwa majumbani mwao pamoja na kunawazawadia kwa kuwapatia unit za Luku za ziada za bure”.
Aliongeza kwa kusema “ Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu zinazokithi na kutatua mahitaji ya wateja wetu , tukiwa na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 45,000 nchini , wateja wetu wanafaidika na huduma ya mikopo, huduma za kuhamisha pesa, kutoa na kuweka pesa na nyingine nyingi.
Huduma ya Airtel Timiza inayotoa mikopo isiyo na dhamana kupitia simu za mkononi ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma za kisasa zenye ubunifu kwa watanzania.” aliongeza Mmbando.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI