DK KAMANI ATANGAZA NIA YA KGOMBEA URAIS 2015


WAZIRI wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Busega (CCM), Dkt.Titus Kamani (pichani) ,amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania,Serikali yake itadhibiti kodi sumbufu na haitakuwa na suluhu na wala rushwa.

Pia, ataboresha sekta ya afya kwa kujenga utamaduni wa kuwa na vifaa tiba na vitendanishi , kujenga uwezo wa wataalamu wa kutosha  ili kupunguza safari za  wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi,ili wageni nao waje kutibiwa nchini .

Dkt.Kamani alitoa  kauli hiyo jana jijini Mwanza , kwenye ukumbi wa Mahatma Ghandhi wakati akitangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) .

Alisema anafahamu kazi na majukumu ya urais ni magumu na wajibu mkubwa,yanahitaji uadilifu na usikivu na kumwoga Mungu,hivyo hatabadilika katika kutoa uamuzi mgumu kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania .
“Ni siku muhimu ya kufanya maamuzi ya kuendesha nchi na kitakachosemwa hapa kitaboresha maslahi ya taifa letu.Tunajitokeza kuomba ridhaa hiyo nchi ikiwa na amani tunapoelekea kubadilisha uongozi wa juu wa nchi yetu,”

“Nakuja kuendeleza kazi ya walionitangulia ,nikianza na serikali ya awamu ya kwanza,Tanzania ilibadilika kutoka vidogo vidogo vya ukabila ,ndiyo misingi iliyowekwa  na Mwl Nyerere.Awamu ya pili uchumi wetu uliyumba, Mwinyi akabadili mfumo na kufungua milango, kazi hiyo ilikuwa ngumu lakini yenye manufaaa kwa nchi yetu ,”alisema Dkt. Kamani

Alisema kuchukua misingi hiyo iliyoachwa na viongozi waliomtangulia kwa ajili ya kuiboresha na kuipeleka nchi yetu katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Serikali ya awamu ya iliimarisha uchumi kwa kujenga miundo mbinu ya usafiri ,uimarishaji wa elimu ya ufunguzi wa Vyuo Vikuu.Awamu ya nne imejenga miundombinu ya kuunganisha mikoa na wilaya,shule za kata na ujenzi wa vyuo Vikuu kikiwemo UDOM na sasa injenga chuo cha kisasa cha tiba za binadatmu,”Alisema Kamani
Aidha wakati Dkt Kamani wakati akitangaza nia yake,  mvua zilikuwa zikinyesha ,jambo ambapo mmoja wa wazee wa wilaya ya Busega,na kamanda wa UVCCM wilayani humo, Emmanuel Mbiti ( 68),alisema kitendo hicho ni ishara njema kwa mtangaza nia huyo.

Alidai kwa mila na imani za kabila la Wasukuma, kitendo cha mvua kunyesha ukiwa unaomba jambo lolote hasa uongozi ,ni ishara njema ya kukubaliwa , hivyo Dkt. Kamani atafanikiwa katika nia yake hiyo.

AJIRA
Alisema anaomba nafasi hiyo huku akifahamu kuwa changamoto hiyo imesababishwa na mafanikio ya elimu,yamezaa tatizo na la ajira ambalo serikali yake lazima ilitizame kwa umakini.
MAJI
Alisema kuwa ili kuimarisha sekta ya maji,na kuongeza kasi ya upatikanaji wake wananchi watawezeshwa kwa kupewa mbinu ya kuvuna maji, kujenga na kuimarha  mabwawa na malambo kwa kiwango cha kutoka mita 400 za ujazo.
Dkt.Kamani alisema kuwa, migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, imekuwa wimbo wa taifa,linatokana na urasimu wa wataaalmu wa idara za mipango miji na hilo halihitaji fedha za kigeni.Kwamba hata maeneo ya makazi na ujenzi holela  ni changamoto kwa sababu hakuna matumizi bora ya ardhi.

RUSHWA

Dkt.Kamani , alisema serikali yake endapo atashinda kiti cha Urais,itadhibiti kodi sumbufu zinazokatisha tamaa na kusababisha wananchi wakose uvumilivu,lazima iliangalie kwa umakini na bila kudhibiti rushwa nchi itaangamia.
Alidai Takukuru itawezeshwa ili ifanye kazi zake vizuri,ili wananchi washiriki kuikomesha rushwa,lakini ili kuimarisha mapato ya serikali na kupunguza  udokozi wa mali ya umma na kamua kamua ya kodi inayofanywa na watumishi wasio waadilifu serikali itaboresha maslahi yao.
“Lazima viongozi waichukie na kuiondoa rushwa hata kwa kuwaangalia usoni, mawazo haya siyo mapya bali  yapo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM


Migogo ya ardhi
 Dkt .Kamani alisema ataiongezea meno Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa hesabu za Serikali (CAG) ili kutoupa nafasi mchwa unaokula na kutafuna fedha za walipa kodi na kukwamisha maendeleo.
“Uzalendo utarejeshwa kwa wananchi, mchwa na unaotafuna  fedha za umma hautakuwa na nafasi katika serikali yangu,wananchi lazima wahakikishiwe mrejesho wa jasho lao na lazima moyo wa uzalendo wa watanzania urejeshwe,”alisema
 Diplomasia ya Kimataifa

Alisema kuwa serikali yake itajenga na kuendeleza urafiki  na mataifa ya nje na kuziwezesha balozi zitafute miradi ya uwekezaji  na hayo yote nyanahitaji rasilimali fedha.

Alisema serikali inahitaji kujitegemea  kwa kuongeza maduhuri na makusanyo ya kodi kutokana na vyanzo mbalimbali ili kuondokana na misaada yenye masharti na bajeti tegemezi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu itakayowezesha kuongeza mapato ya serikali.

Kuhusu Sekta ya uchukuzi na biashara atajenga bandari kubwa na reli kwa ajili ya kusafiri mizigo na bidhaa kwenda nchi jirani za Burundi ,Rwanda na Congo DRC ,ambapohi  ataweka mfumo mzuri wa utoaji huduma na kuondoa urasimu uliopo bandarini.

Alisema katika sekta ya uwekezaji ,serikali yake itahakikisha v inajenga na kuimarisha viwanda vikubwa , vidogo na vya kati ili kuongeza thamani ya mazao badala ya kuuza nje yakiwa ghafi.

Pia ataondoa urasimu wa utoaji vibali kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda kwani unachelewesha kodi inayostahili kulipwa serikalini,lakini pia atakuza  wafanyabiashara wa ndani, kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji.
Alisema ataunda serikali ndogo ambapo maamuzi mengi yatafanywa na serikali za mitaa na zitawezeshwa ili zitimize wajibu wake.ataweka mfumo rafiki wa uendeshaji kilimo kwani hakiwezi kuendeshwa kwa fedha za mfukoni,bali mikopo kutoka katika taasisi za fedha ukizingatia kilimo ni uti wa mgongo wan chi yetu

Alisema skta ya madini,itaangliwa ili kuona serikali yake inapata mapato yanayoendana na uzalishaji,lakini pia itashughulika na wachimbaji wadogo wadogo kwa kutambua kazi zao,ikiwa ni pamoja na kuongeza madini yao thamani badala ya kuuza madini ghafi.
mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI