HABARI LUKUKI KUTOKA TFF

STARS YAJIFUA ADDIS ABABA
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhamini na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo imeanza mazoezi katika uwanja wa  Addis Ababa zamani ukifahamka kama (Haille Sellsie) uliopo jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 14, jijini Alexandria.

Stars ambayo iliwasili jana jioni jijini Addis Ababa imefikia katika hoteli ya Debre Damo iliyopo eneo na 22 Mazoiria ambapo itakaa kambi kwa kipindi cha wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema anashukuru vijana wake wamefika salama, na wapo katika hali nzuri, anaamini wiki moja ya maandalizi nchini Ethiopia itasaidia kikosi chake kuwa fiti ajili ya mchezo.

Akiongelea kuhusu kambi, kocha Nooij amesema kwa kuwa mji wa Addis Ababa upo katika ukanda wa juu( mita 2000 kutoka usawa wa bahari), kambi ya mazoezi itakua nzuri kutokana na wachezaji kufanya mazoezi katika hali hiyo na kwenda kucheza katika ukanda wa kawaida.

Kuhusu hali ya hewa ni nzuri kwani baridi iliyopo kwa sasa Addis Ababa ni ya kawaida, hivyo haitaweza kuwasumbua wachezaji katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.

Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa katika jiji la Alexandria ambalo lipo eneo la bahari ya Mediteranian.

NB: Picha za mazoezi ya Taifa Stars leo zimeambatanishwa.

Napatikana kwa namba hii Ethiopia +251 96100 5754


TFF YAWAITA SIMBA, SINGANO JUNI 9 
TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano na klabu ya Simba.

TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Ramadhani Singano wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo.

Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.

Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.