Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisalimiana na Aliyekuwa Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa sasa Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima muda mfupi
kabla ya kuanza kwa hafla ya kumuaga Ndugu Chima na kumkaribisha Ndugu
Smythies Pangisa (katikati) aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara sasa
Mkoa wa Rukwa. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 13 Juni 2015 katika ukumbi
wa Kanyau Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Mwenyekiti
wa Kamati ya maandalizi ya hafla hiyo ambaye pia ni Meneja wa SIDO Mkoa
wa Rukwa Ndugu Martin Chang’a akitoa salam za utangulizi katika hafla
hiyo.
Meza Kuu.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza katika hafla hiyo.
Aliwaasa watumishi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na ubunifu mkubwa na
kwamba ndiyo siri pekee ya mafanikio katika utendaji wao wa kazi.
Katika
hali isiyotegemewa na wengi Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Alhaj Salum
Chima “Muagwa” alitoa zawadi ya machungwa kutoka Tanga ambayo yaligawiwa
kwa washiriki wote wa hafla hiyo kama inavyoonekana pichani.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa katika hafla hiyo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akizungumza katika hafla
hiyo. Kabla ya hapo alikua Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
Katibu
Tawala Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima wa pili kushoto akionyesha
umahiri wake wa kucheza ngoma ya kinyaturu na baadhi ya wanakikundi wa
ngoma hiyo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Tanga Alhaj Chima na Mkoa wa Rukwa Ndugu Pangisa
wakipokea zawadi kutoka kwa Watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
Washiriki wote katika hafla hiyo walipata fursa ya kupeana mikono na Makatibu Tawala hao wa Mkoa wa Tanga na Rukwa.
Watumishi waliofanya kazi kwa karibu zaidi na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima wakikabidhi zawadi zao.
Picha ya Pamoja kati ya wageni wa meza kuu na wakuu wa idara Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)
Comments