KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD KWA MWAKA WA TATU MFULULIZO YASHIKILIA TUZO YA UBORA ,YAZIBWAGA KAMPUNI KONGWE TENA WAZIRI KAMANI APONGEZA



Afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu (kulia)  akiwa na   wafanyakazi  wenzake baada ya  kutwaa tuzo ya ubora ya Kitaifa katika  bidhaa za Asas Dairies Ltd 

Hii  ndio kampuni  iliyoweza  kushinda tuzo ya  ubora
Medali  ,vyeti na  tuzo  ya ushindi  ambayo kampuni ya Asas Dairies Ltd imeshinda  tena  mwaka huu katika maonyesho ya maziwa mkoani Mara

Vyeti na medali  tatu  ambazo kampuni   ya Asas Dairies Ltd imeshinda  tena kwa
Baadhi ya  bidhaa za kampuni ya Asas Dairies Ltd zilizoshinda medali 

Na Matukiodaima Blog
BIDHAA na maziwa yanayotengenezwa na kampuni ya  Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa kwa  mwaka  wa tatu  mfululizo  zimeendelea kushikilia tuzo ya ubora na  kuwa kampuni  bora kuliko  makapuni mengine ya maziwa hapa nchini .

Kampuni hiyo  ya   Asas Dairies Ltd ambayo ni  moja kati ya makampuni ya  kizalendo nchini na moja kati ya makampuni yaliyopata  kupewa  tuzo  ya ulipaji  kodi mzuri na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imeshinda katika maadhimisho ya wiki ya maziwa mwaka  huu tena yaliyofanyika wilaya Babati mkoani Mara kwa  kushindanisha kampuni  zaidi ya 20 .

 Akizungumzia ushindi  huo afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu  alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuongoza kwa mwaka  huu wa tatu mfululizo bado  bidhaa  zake  nyingine  zimeendelea  kushinda medali mbali mbali na kuonyesha uwezo mkubwa wa kampuni  hiyo katika ubora .

Alisema baadhi  ya makampuni makubwa ambayo  yalipata  kuingia  katika mashindano  hayo ni  pamoja na Tanga Fresh, DarFresh,Kilimanjaro Fresh,Creamer Fresh,Cefa, Grand DeMom ya Engingteng, Nansinya ya Arusha  ,Nnronga  ya Kilimanjaro mengine  mengi.

 Alisema kuwa bidhaa  kwa  mwaka  huu kila kampuni  lilikuwa likishindanisha bidhaa zake tatu huku kampuni  yake Asas Dairies Ltd bidhaa  zake  zote  tatu  zilishinda na kupewa medali .

Pamoja na kushinda katika bidhaa hizo bado kampuni  hiyo ilinyakua  tuzo ya  jumla katika  ubora .

 Bw   Kiwelu  aliwataka  watanzania kuendelea  kuzipenda  bidhaa za Asas Dairies Ltd  kutokana na kuendelea kuongoza katika ubora na kuwa lengo  la kampuni hiyo  kuendelea kushinda  tuzo  za  ubora 

Pia  alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa  wanaombwa  kuihamasisha jamii   kuendelea  kutumia maziwa hayo na  bidhaa nyingine za chini ya kampuni ya kizalendo ya Asas Dairies Ltd 

Bw Kiwelu  alisema mwaka huu  jumla ya Medali 9  zilikuwa  zikishindaniwa ila kampuni  Asas Dairies Ltd iliweza  kuongoza  kushinda medali 3 kati ya 9.

 Aliyekuwa mgeni rasmi tena kwa  mwaka  huu  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani pamoja na  kupongeza mshindi  huyo wa jumla na washiriki  wengine katika maonyesho  hayo bado  alitaka makampuni zaidi  kuendelea  kushiriki maonyesho hayo kwani  yanasaidia  kutambua changamoto katika utengenezaji wa bidhaa bora .

Pia  alieleza  kufurahishwa na hatua  kubwa ya  kampuni  hiyo ya Asas Dairies  Ltd  kwa  kuendelea  kufanya  vizuri katika mashindano hayo ya ubora  wa maziwa nchini na kuwa  mbali ya kuwa ni  heshima ya kampuni na mkoa wa Iringa ila bado ni  heshima kwa Taifa  kuona kamapuni ya ndani yanaonyesha ufanisi  mkubwa katika bidhaa zake .


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA