KOMREDI KINANA AFANYA ZIARA KATIKA VISIWA VINNE WILAYANI MULEBA, AWAPA UHURU WAKULIMA KUUZA KAHAWA KOKOTE KWENYE BEI NZURI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akijadiliana jambo na waziri wa zamani wa Nymba Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye ndani ya boti wakitokea Kyamkwikwi kwenda Kisiwa na Iloba, Kata ya Ibumbile Jimbo la Muleba Kaskazini, mkoani Kagera.

Komredi Kinana yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kuiamarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Muleba Mjini, Komredi Kinana aliwaruhusu wakulima wa zao la kahawa kwenda kuuza kokote nje na ndani ya nchi kwenye bei nzuri ya zao hilo.Kitendo hicho kiliungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongela.

Pia Komredi Kinana alikemea kitendo cha maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kuwanyanyasa wavuvi.


 Komredi Kinana akilakiwa kwa furaha na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka baada ya kuwasili katika Kijiji cha Kyamkwikwi Wilaya ya Muleba, Kagera.
 Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini, Charles Mwijaga akielezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa jimboni humo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi
 Komredi Kinana akiwa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Mkutano Mkuu wa Taifa, Ambrose Mshala (kushoto) pamoja na Mbunge wa Muleba Kusini. Anna Tibaijuka wakielekea kupanda boti katika Kijiji cha Kyamkwikwi kwenda ziara katika visiwa vinne katika Ziwa Victoria
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Kagera (Revina Jovin (kushoto) akiwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana, bw. Edward ndani ya boti wakati wa kwenda katika visiwa vinne wilayani Muleba.

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba, leo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na uhai wa Chama katika wilaya hiyo mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya yeye na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba, leo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na uhai wa Chama katika wilaya hiyo mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimsikiliza kwa makini, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofayika kijiji cha Katunguru, wilayani Muleba leo
 Wananchi wa kijiji cha Katungulu wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowahutubia akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kukagua uhai wa CCM, mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika Kijiji hicho cha Katunguru. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi katika kijiji hicho cha Katunguru
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdlrahman Kinana akiwasili katika Uwanja wa Mpira wa Muleba Mjini, kuhutubia mkutano wa hadhara leo mchana
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdlrahman Kinana akiwasili katika Uwanja wa Mpira wa Muleba Mjini, kuhutubia mkutano wa hadhara leo mchana
 Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka  akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
  KTIBU  NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
 Uwanja wa mpira wa Muleba mjini, ukiwa umefurika wananchi wakati Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja huo
 
Mjumbe wa Baraza la Vijana Utekelezaji Taifa, Halima Bulembo (laiyekaa amevaa kilemba) akiwa miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM mjini Muleba.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,  akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
 Katibu Mkuu wa CCM, akikabidhi cheti kwa mmoja wa maderefa wa bodaboda ambao wameshiriki mafunzo ya kuendesha bodaboda ambayo yaliratibiwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka. Kinana alikabidhi vyeti hiyo katika mkutano huo wa hadhara
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini mkazi mmoja wa Muleba mjini, ambaye alikuwa na kero ambayo alitaka Chama Cha Mapinduzi kimsaidie kulitatua













Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Profesa Anna Tibaijuka wakiwa na vijana wa bodaboda waliopewa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.