KOMREDI KINANA AHITIMISHA ZIARA MKOA WA GEITA, ATUMIA USAFIRI WA GARI KM 1680, AHUTUBIA MIKUTANO 78 NA KUKAGUA MIRADI 53

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Nyamkumbu, Kata ya Katangalala, wakati wa ziara yake mkoani Geita ya Kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye leo wamehitimisha ziara ya siku sita mkoani Geita, ambapo wamesafiri kwa umbali wa km 1680 kwa magari na kuhutubia mikutano 78 sita ikiwa ya ndani. Amekagua miradi 53 ambapo 48 ya maendeleo na mitano ya CCM.

Katika ziara hiyo mkoani Kagera wamejikusanyia jumla ya wanachama wapya 6816 wakiwemo wa upinzani 640. Akiwa mkoani Geita tayari amefanya ziara katika majimbo ya Chato, Bukombe, Mbogwe, Nyang'hwale, Busanda na Geita yenyewe.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano hadhara kwenye Uwanja wa Nyankumbu, Kalangalala, jimbo la Geita, ambapo amewataka viongozi wa Serikali waanze kutoka maofisini kwenda kuwatembelea wananchi na kutatua kero zao ama kama hawataki basi waachie nafasi walizonazo warudi kucheza na watoto na wake zao.
 Komredi Kinana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ibrahim Marwa wakishiriki kujenga paa ya nyumba Mganga katika Kata ya Nyanguku wilayani Geita.
 Komredi Kinana akizungumza baada ya kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga katika Kata ya Nyanguku.
 Komredi Kinana akishiriki kupiga ripu katika jengo la Shule ya Sekondari ya Ihanamilo, Jimbo la Geita.
 Mmoja wa watoto pacha akiimba wimbo wa kuisifia CCM na Komredi Kinana wakati Kinana aliposhiriki ujenzi wa jengo la sekondari ya Ihanamilo, wilayani Geita.

 Nape akiwa amewabeba watoto pacha baada ya kufurahishwa baada ya kuimba vizuri wimbo wa kuisifu CCM na Komredi Kinana katika Shule ya Sekondari ya Ihanamilo wilayani Geita.
 Watoto hao pacha wakisalimiana na Komredi Kinana baada ya kupelekwa na Nape.
 Wachimbaji wadogo wadogo wa madini wakisafisha udongo kupata dhahabu katika machimbo ya Mgusu, wilayani Geita.
 Akina mama wanaofanyakazi katika mgodi wa wachimbaji wadogowadogo wa madini, wakipasua mawe yenye chembechembe za madini
Komredi Kinana akishiriki kupasua mawe alipokwenda kukagua Mgod i  ya dhahabu wa madini wa wachimbaji wadogowadogo wa Mgusu, wilayani Geita.
 
 Komredi Kinana akikagua mgodi wa Mgusu, wilayani Geita.
 Komredi Kinana akipata maelezo jinsi udongo wenye dhahabu unavyochujwa katika Mgodi wa Mgusu, wilayani Geita.
 Komredi Kinana akioneshwa jinsi dhahabu inavyopimwa kwenye mizani ndogo
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Komredi Kinana alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu katika Mji wa Mgusu.
 Komredi Kinana akipaka rangi jengo la Zahanati ya Nyamilyango, wilayani Geita
 Wananchi wakishiriki pamoja na Komredi Kinana kutandaza waya wa umeme wa REA katika Kijiji cha Kasota, wilayani Geita.
 Kinana akisalimiana na wananchi katika Kijiji cha Nzera, wilayani Geita
 Wananchi wakishuhudia Komredi Kinana akifungua Jengo la Ofisi Kata ya Nzera, wiayani Geita.
 Komredi Kinana akishiriki kufukia mabomba ya maji eneo la Shilabela, Kata ya Kalangalala, wilayani Geita.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ibrahim Marwa akizungumza katika kiutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Nyamkungu Kalangalala, mjini Geita.
 Kinana akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mhandisi wa Maji wa Mamlaka ya Maji Geita, Clemence Chagu akilelezea mipango ya maji ilivyo katika Mji wa Geita.
 Sehemu ya umati wa wananchi kwenye mkutano uliohutubiwa na Komredi Kinana
Komredi Kinana akikusanya kadi za wanachama mbalimbali wa vyama vya upinza walioamua kuhamia CCM wakati wa mkutano wa hadhara mjini Geita.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU