KOMREDI KINANA AHITIMISHA ZIARA YA MIKOA 38, ASAFIRI KWA MAGARI KM 200,000

 Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. Mkutano huo umefanyika kwenye viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.

Komredi Kinana ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, tayari wamesafiri umbali Km 193,537, kwa kufika katika Wilaya 163, majimbo 239, nusu ya vijiji na kata 1938 za Tanzania.

Pia msafara wake ulitumia jumla ya saa 84 kuzunguka mikoa yote hiyo, na kusafiri kwa mitumbwi katika visiwa 16.

Amehutubia jumla ya mikutano ya ndani/hadhara 1918 na kujikusanyia wanachama wapya 284300 ambapo kutoka upinzani 38984.
 Komredi Kinana akiwapungia mkono wananchi alipokuwa wakiwasili kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, ambapo aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa kuwa bunge lijalo kwa upande wa CCM, litakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali kuhusu utendaji wake.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CCM kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza leo
 Komredi Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza leo, ambapo amewataka viongozi wa chama na Serikali kutoka maofisini kwenda kwa wananchi kuzitafutia ufumbuzi kero zao.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  akihutuia katika mkutano huo, ambapo amewahakikishia wananchi kwamba CCM itashinda katika uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu, hivyo kuingia Ikulu.
 Wananchi wakishangilia hotuba ya Komredi Kinana.
 Nape akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika mkutano huo wa hadhara
 Mrithi wa uimbaji wa aliyekuwa kiongozi wa Kikundi cha Sanaa cha CCM cha Tanzania One Theather (TOT), marehemu Jihn Komba  akiwa na Malkia wa Mipasho wa kikundi hicho, Khadija Kopa wakati kikundi hicho kilipokuwa kikitumbuiza kwa kawaya wakati wa mkutano kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza leo.
 Komredi Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
 Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Komredi Kinana

 Waliokuwa wanachama wa vyama vya upinzania wakikabidhi kadi zao kwa Komredi Kinana walipoamua kuhamia CCM kwenyemkutano wa hadhara uliofanyika  Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza leo
 Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Chadema kupitia Chadema, Opulukwa akikaribishwa CCM na Komredi Kinana baada ya kuamua kukihama chama chake na kujiunga na CCM
 Sehemu ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo
Baadhi ya kadi zilizotolewa na waliokuwa wananchama wa vyama vya upinzani na kuamua kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.