KOMREDI KINANA ASHIRIKI KUOGESHA MIFUGO WILAYANI NYANG'HWALE

 
 Katibu Mkuu wa CCM , aAbdulrahman Kinana akiwa amebeba mbuzi akimpeleka kwenye josho  katika Kijiji cha Nyakwasi wakati wa ziara yake wilayani Nyang'hwale, Geita ya kuimarisha Uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

 Komredi Kinana akiswaga ng'ombe ili waende kwenye josho katika Kijiji cha Nyakwasi, wilayani Nyang'hwale, mkoani Geita.
 Komredi Kinana akimtumbukiza mbuzi kwenye josho, katika Kijiji cha Nyakwasi, wilayani Nyan'hwale, Geita.Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale, Hussein Kasu ameshiriki ujenzi wa josho hilo pamoja na malambo 91 jimboni humo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Komredi Kinana akiswaga ng'ombe ili waingie kwenye josho kwa ajili kuua wadufu katika Kijiji cha Nyakwasi wilayani humo.
 Komredi Kinana akilakiwa katika Kijiji cha Bukwimba, ambapo alishiriki kupaka rangi jengo la CCM Kata ya Bukwimba,
 Komredi Kinana akishiriki kupaka rangi jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Bukwimba wilayani Nyang'wale. mkoani Geita.
 Komredi Kinana akishiriki kufukia mabomba ya maji katika Kata ya Bukwimba, wilayani Nyang'hwale, Geita.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Busolwa, ambapo Komredi Kinana alikagua ujenzi wa Daraja  katika Kitongoji cha Mwiza, wilayani Nyang'hwale.
 Komredi Kinana akiwasha mashine za kusaga na kukoboa mradi wa akina mama wa Kijiji cha Nyangongwa, wilayani humo
 Komredi Kinana akiwasili katika Kijiji cha Busolwa mbapo alikagua ujenzi wa daraja  katika kitongoji cha  Mwiza Kijiji cha Busolwawilayani Nyang'hwale
 Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji Busolwa wilayani humo.
 Wananchi wa Kijiji cha Busolwa wakimsikiliza kwa makini Komredi Kinana alipokuwa akizungumza nao baada ya kukagua ujenzi wa daraja lililogharamiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Husein Kasu.

 Komredi Kinana akiangalia kabeji iliyozalishwa na kikundi cha akina mama wa Kijiji cha Nyang'hwale, wilayani humo, wilayani humo.
 Komredi Kinana akizindua jengo la kitega uchumi la CCM Kharumwa, wilayani Nyang'hwale
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Hussein Kasu (kushoto) na Mjumbe wa NEC James Msalilwa walipokuwa wakielekea kukagua ujenzi wa wodi ya wazazi na watoto katika Hospitali ya Wilaya, ujenzi ambao ulifadhiliwa na Mbunge wa Jimbo hilo.
 Komredi Kianana akitoka kukagua ujenzi wa jengo hilo la wodi za Wazazi na watoto katika Hospitali ya Wilaya hiyo.
 Komredi Kinana akiangalia ngoma alipowasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Kharumwa, wilayani Nyang'hwale.
 Wananchi wakishangilia baada ya kumuona Komredi Kinana alipowasili kuhutubia katika mkutano huo wa hadhara.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ibrahim Marwa,  akihutubia katika mkutano huo
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo ambapo alisema tusiwaruhusu wapinzania wanaotaka kuharibu amani ya nchi yetu.

 Komredi Kinana  akihutubia katika mkutano wa hadhara Makao Makuu ya Wilaya Nyang'hwale


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA