KOMREDI KINANA ATINGA WILAYA YA MISUNGWI, MWANZA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la dengu la mwaanchi katika Kijiji cha Misasi wakati wa ziara ya wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza ya  kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.

Komredi Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ametokea wilayani Sengerema, baada ya kumaliza ziara katika mikoa ya Kagera na Geita.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (katikati), akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja (kulia), pamoja na  Katibu wa CCM, Mkoa wa Mwamza, Mirald Mtatiru. walipokuwa wakisubiri kupanda Kivyko cha MV Misungwi, eneo la Busisi. Sengerema kwenda kuanza ziara wilayani Misungwi leo.
 Komredi Kinana na viongozi wengine wa chama hicho wakipanda kivuko cha Mv Misungwi akitokea Sengerema kwenda Jimbo la Misungwi, mkoa wa Mwanza kuendelea na ziara.
 Komredi Kinana akijadiliana jambo  na viongozi wa CCM ndani ya Kivuko cha Mv Misungwi.

 Komredi Kinana akiwa na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (kushoto) pamoja na Katibu wa Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu wakishuka kwenye Kivuko cha Mv Misungwi wakitokea Wialaya ya Sengerema kwenda Misungwi.
 Komredi Kinana  (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wakitoka katika Kivuko cha Mv Misungwi.
 Msafara wa Komredi Kinana aukitoka katika Kivuko cha Mv Misungwi kuendelea na ziara Jimbo la Misungwi.
 Wasanii wa ngoma za asili wakishangilia kwa furaha wakati wa kumlaki Komredi Kinana katika Kijiji cha Usagara, wilayani Misungwi.
 Komredi Kinana akiangalia ngoma iliyokuwa ikitumbuiza  wakati ya mapokezi  yake katika Kijiji cha Usagara, wilayani Misungwi.

 Wasanii wa ngoma ya asili wakishangilia wakati wakimlaki Komredi Kinana wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza leo.
 Komredi Kinana akishiriki kuweka fremu ya dirisha katika Zahanati ya Nyang'omango, wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza leo.


 Komredi Kinana akipandisha bendera ya CCM, baada ya kufungua ofisi ya  Tawi la Nyang'omango, wilayani Misungwi.
 Akina mama wakiburudisha kwa ngoma za asili wakati Komredi Kinana alipokwenda kuzungumza na wananchi kujua changamoto zinazo wakabili na kuzitafutia ufumbuzi katika Kijiji cha Misasi, wilayani Sengerema. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Komredi Kinana akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Misasi, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Misungwi.
 Komredi Kinana akilakiwa ngoma za asili alipowasili katika  katika Kijiji cha Mahando kuweka jiwe la msingi ujenzi wa kitega Uchumi cha CCM, WILAYANI mISUNGWI.
 Komredi Kinana akifunua pazia ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya CCM ya Tawi la mahando, wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza.
 Vijana wakishangilia ujio wa Kinana  huku wakimfagilia na kumtaka Mbunge wao  Charles Katwanga kwamba anafaa  kugombesa tena ubunge wa j
 Komredi Kinana na msafara wake wakiingia katika moja ya vibanda vya mama ntilie katika Soko la Misungwi alipokwenda kuwatembelea.
 Komredi Kinana akiwa katika moja ya vibanda vya mama ntilie wakati wa ziara yake Misungwi mjiui.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo alisema kuwa vyama vya upinzani vitakufa kwa vile havina hata ajenda ya kusaidia maendeleo ya wananchi.
 Bibi kizee Hadija Abdalah (96), akisikiliza kwa makini wakati Komredi Kinana akihutubia wananchi mjini Misungwi wakati wa ziara yake mkoani Mwanza.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Misungwi leo.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Misungwi ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa atasaidia wachimbaji wadodgo wadogo kupata vitalu vya kuchimba madini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.