KOMREDI KINANA ATUA KIJIJI CHA RUSHWA, MULEBA KASKAZINI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa nne kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Anna Tibaijuka ( wa tatu kushoto)  pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongela (kushoto), wakishiriki katika kazi za utandazaji wa umeme wa REA katika Shule ya Sekondari ya Nyakatanga, Jimbo la Mule Kaskazini, mkoani Kagera wakati wa ziara ya kuiamarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

 Komredi Kinana akihutubia baada ya kukagua mradi wa maji wa Kata ya Nshamba, Jimbo la Muleba Kusini, mkoani Kagera.
 Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akihutubia katika kutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Nshamba.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika Kata ya Nshamba, wilayani Muleba, Kagera, ambapo alisema kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu vyama vya upinzani vitasoma namba kwani vitashindwa kabisa.
 Komredi Kinana (kushoto) akihutubia katika mkutano  wa hadhara katika Kata ya Nshamba wilayani Muleba,
 Komredi Kinana akikata utepe kuzindua rasmi chumba cha darasa la kompyuta katika Shule ya Skondari Nyakatanga, wilayani Muleba, mkoani Kagera.

 Wananchi wakimlaki Komredi Kinana alipowasili katika mkutano uliofanyika katika Kitongozji cha Rushwa, Kata ya Mushabago, Jimbo la Muleba Kaskazini linaloongozwa na Mbunge Charles Mwijage.
 Diwani wa Chadema wa Kata ya Mushabago, Respikius Feruz (aliye vaa tai)akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage ambaye alitoa hotuba nzuri ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata hiyo na jimboni kwa ujumla.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Rushwa, Jimbo la Muleba Kaskazini, ambapo alimsifia Mbunge wa Jimbo hilo, Charles  Mwijage.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kamachumu, Jimbo la Muleba Kaskazini
 Mzee wa Kata ya Kamachumu, akielezea mbele ya Komredi Kinana jinsi wakulima wa kahawa wanavyonyanyasika na vyombo vya dola kwa kuwakamata mara kwa mara wanapouza kahawa yao Uganda, ambako bei yake ni kubwa  kuliko bei ya Tanzania. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Komredi Kinana akikabidhi baiskeli kwa makatibu wa CCM zilizotolewa msaada na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini.

 Komredi Kinana akikabidhi jenereta
 Wajasiriamali wakionesha samaki waliovuliwa katika mradi wa ufugaji wa samaki wa Ruhanga katika Jimbo la Muleba Kaskazini.
 Komredi Kinana akiwa na Profesa Tibaijuka wakikagua mabwa ya ufugaji wa samaki  wa Ruhanga.
Bwawa moja huzalisha samaki ambao kwa miezi sita wanaweza kuu za samaki wenye thamani ya sh. milioni 35.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Izigo, Jimbo la Muleba Kaskazini.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara  katika Kijiji cha Izigo, Muleba Kaskazini.
 Komredi Kinana akihutubia katika Kijiji cha Izigo, Jimbo la Muleba Kaskazini.
 Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chadema Wilaya ya Muleba (Alex Damian (wa pili kulia) akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Izigo, Muleba Kaskazini. (wa pili kushoto ni Honolaco Charles kutoka Chadema ambaye pia alitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*