KOMREDI KINANA, NAPE WAUNGURUMA NA KUKEMEA KITENDO CHA WABADHIRIFU WA MALI ZA UMMA KULINDWA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Uhuru Park Mjini Bukoba, mkoani Kagera jana, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Uhuru Park, ambapo aliitaka serikali kuwachulia hatua kali wabadhilifu wa mali za umma bila kujali rangi yake.
 Waendesha Bodaboda wakiongoza msfara wa Komredi Kinana ulipoingia leo asubuhi mjini Bukomba.
 Mmoja wa waendesha bodaboda akifanya minjonjo wakati wa mapokezi ya msafara wa Komredi Kinana mjini Bukoba leo
 Komredi Kinana akihutubia wakati wa uzinduzi wa ofisi ya kikundi cha wamachinga mjini Bukoba leo, ambapo pia aliendesha haramee ya kutunisha mfuko wa kikundi hicho.

 Komredi Kinana akihutubia katika Soko Kuu ya Manispaa ya Bukoba, ambalo linatarajiwa kujengwa upya.
 Komredi Kinana akiwa na mmachinga aliyekutana naye kwenye soko lKuu la mjini Bukoba.
 Komredi Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Julius Muungwana kuhusu ujenzi wa Uwanja huo ambao kwa asilimia kubwa umekarabatiwa .
 Komredi Kinana akikagua ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba
 Komredi Kinana akikagua sehemu ya abiria kuchukulia mizigo mashine ambayo inaendeshwa kwa umeme.
 Komredi Kinana akisindikizwa alipokuwa akitoka kukagua uwanja huo
 Wananchi pamoja na wafanyabishara wakimsikiliza kwa makini Komredi Kinana alipokuwa akiwahutubia  baada ya kupata taarifa ya mipango ya ujenzi wa Soko la Kashai, mjini Bukoba.
 Komredi Kinana akipata taarifa kuhusu chanzo cha maji katika Kijiji cha Bunkango, Morogoro mjini.
 Kinana akitoka kukagua chanzo cha maji  Mtaa wa Bunkango
 Komredi Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Balozi Hamis  Kagasheki 'Swahiba' pamoja na Nape
 Komredi Kinana (kulia) akishiriki katika ukarabati wa barabara katika unaofanywa n kwa nguvu za wananchi katika Mtaa wa Lubumba, Kata ya Nyanga, Jimbo la Bukoba Mjini.
 Nepe akijadiliana jambo na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile walipokutana  wakati wa ziara katika Kata ya Nyanga alipozaliwa Balile.. Balile anaishi Dar es Salaam.
 Komredi Kinana na Nape wakizungumza na mmoja wa makada vijana wa CCM katika Kata ya Nyanga.
 Komredei Kinana akishiriki ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Lwomunda katika Kata ya Nyanga, Bukoba.
 Akinana mama wajasiriamali wakifurahia hotuba ya Komredi Kinana aliyekwenda kuzindua kikundi chao eneo la Forodhani Bunena Bukoba mjini.
 Komredi Kinana akiwa na wakandarasi wa mraddi mkubwa wa maji, alipkwenda kukagua maendeleo ya ujenzi mjini Bukoba
 Wananchi wakishangilia  wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Komredi Kinana kwenye Uwanja wa Uhuru Park
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongela akihutubia katika mkutano huo wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Bukoba, Kagasheki akifurahi pamoja na wafuasi wa CCM wakati wa mkutano huo wa hadhara

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA