KOMREDI KINANA, NAPE WAUNGURUMA WILAYANI CHATO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Chato,mkoani Geita,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye,akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini
Chato, Mkoa wa Geita,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Komredi Kinana akikagua gwaride la Chipukizi wa CCM, alipowasili katika Kata ya Kasenga, wilayani Chato, alipoanza ziara katika Mkoa wa Geita, baada ya kumalizaziara katika Mkoa wa Kagera jana.
 Komredi Kinana akikata utepe kuzindua rasmi Ofisi ya CCM Kata ya Kazunguti, wilayani Chato.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kazunguti, wilayani Chato.
 Komredi Kinana akizindua mitambo ya kusukuma maji katika mjini Chato.
Komredi Kinana akikagua mitambo hiyo ya kusukuma maji
  Komredi Kinana akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha ujasiriamali ya Kilimani baada ya kuzindua mitambo ya kusukuma maji mjini Chato.
 Komredi Kinana akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa  Chato yaliyotekwa kwenye bomba wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wilayani Chato

 Komredi Kinana akimkabidhi cheti cha hisa mmoja wa wanahisa wa kikundi cha Saccos cha Mshikamano mjini Chato.
 Komredi Kinana akishiriki kutandaza waya katika mradi wa umeme vijijini (Rea) katika Kata ya Mkungo, wilayani Chato.

 Wananchi wa Kijiji cha Kurugusi, wilayani Chato wakiwa na mabango walipozuia msafara wa Komredi Kinana ili wapatiwe ufumbuzi wa kupatiwa umeme ambao nguzo zake zimepita katika kijiji hicho. Kinana aliwahakikishia kupta umeme huo wa REA,
 Komredi Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji hicho cha Kurugusi baada ya kuelezwa tatizo la kutopatiwa umeme licha nguzo kupita katika kijiji hicho.
 Komredi Kinana akiagana wananchi wa kijiji hicho baada ya kuzungmza nao na kuahidi kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
 Komredi Kinana akiangalia ngoma ya asili iliyokuwa ikitumbiza alipowasili katika Kata ya Ihanga, kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wilayani Chato.
 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wa zahanati ya Kata ya Ihanga, wilayani Chato.
 Kinana akitoka kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wa Zahanati ya Ihanga.
 Wananchi  wakimsalimia Komredi Kinana alipowasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Chato
 Kinana akiingia kwenye mkutano wa hadhara mjini Chato
 Wasanii wanaocheza pamoja na fisi wakitumbuiza mbele ya Komredi Kinana kwenye mkutano huo wa hadhara mjini Chato.
 Kwaya ya Amani ikitumbuiza wakati wa mkutano huo.
 Mjumbe wa NEC  kutoka wilaya ya Chato, Deusdedit Katwale akihutubia katika mkutano huo ambapo alimuomba Komredi Kinana kuwasaidia kuinua maisha ya waendesha bodaboda mjini Chato. Yeye alichangia pikipiki moja.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo akijitambulisha kwa wananchi wakati wa mkutano huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA